Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kibwana bado yupo yupo sana

New Content Item (2)
New Content Item (2)

Muktasari:

  • Kibwana ambaye ameitumikia Yanga kwa miaka mitatu tangu ametua akitokea Mtibwa Sugar, ataendelea kubaki zaidi ndani ya timu hiyo ya Jangwani kwa miaka mingine miwili.

UONGOZI wa klabu ya Yanga, umemuongeza mkataba wa miaka miwili beki wao wa kulia, Kibwana Shomari kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Kibwana ambaye ameitumikia Yanga kwa miaka mitatu tangu ametua akitokea Mtibwa Sugar, ataendelea kubaki zaidi ndani ya timu hiyo ya Jangwani kwa miaka mingine miwili.

Beki huyo ambaye ametwaa mataji mawili ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho (FA) anaendelea kupambania nafasi mbele ya Kouassi Attohoula Yao ambaye amekuwa panga pangua katika kikosi cha kwanza tangu ametua akitokea ASEC Mimosas.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kimeliambia Mwanaspoti kuwa lilikuwa ni suala la muda kwa beki huyo kuongeza mkataba kutokana na uwezo aliouonyesha tangu ametua akitokea Mtibwa Sugar.

"Hatuwezi tukawa na beki mmoja wakati tuna mashindano mengi ya ndani na nje hivyo kuhusu kumuongeza mkataba Kibwana lilikuwa ni suala la muda tu sasa mambo yamekamilika," kilisema chanzo hicho.

Hadi sasa, mastaa walioongezwa mikataba Yanga ni Djigui Diarra, Farid Mussa, Abuutwalib Mshery, Bakari Mwamnyeto, Jonas Mkude na Salum Abubakar 'Sure Boy'.