Kibu atawafunga sana

Muktasari:

MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Kibu Denis ni miongoni mwa wachezaji wapya ambao juzi kwenye Simba Day walikiwasha kinoma na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo kumtabiria makubwa huku mwenyewe akisema ule ni mwanzo tu.

Kibu alisainiwa na Simba akitokea Mbeya City na juzi alianza kwenye kikosi cha kwanza cha Mnyama dhidi ya TP Mazembe na kuonyesha kiwango bora akicheza sambamba na Chris Mugalu kama washambuliaji.

Baada ya kuanza kazi rasmi Simba, Kibu aliliambia Mwanaspoti kuwa ule ni mwanzo tu na kinachofuata ni kuhakikisha anafanya vizuri na kuwapa furaha mashabiki.

“Nimefurahi kwa mapokezi tuliyopatiwa na mashabiki, kila mmoja anataka kuiona Simba ikifika mbali na nitahakikisha nakuwa sehemu ya kufanikisha hilo,” alisema Kibu.

“Lengo kuu ni kufikia malengo ya klabu, mimi ni mshambuliaji, hivyo kila nikipata nafasi nitaitumia vizuri na kufunga kama ilivyo ndoto ya kila mchezaji.”