Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KIBEGI CHA TICHA: Namungo imepoteza, ila Kaze kashinda kimbinu

ILIKUWA ni shtukizo la kimchezo kwa wale tulioziangalia mechi mbili ilizocheza Namungo kwenye uwanja wa nyumbani, Majaliwa uliopo Ruangwa, mkoani Lindi dhidi ya JKT Tanzania na KMC kwani tukishuhudia kiwango cha chini sana cha uchezaji wa timu hiyo, tukaja kutoa suluhisho kuelekea mchezo dhidi ya Yanga.

Kuna mambo mengi ambayo Kocha Cedric Kaze ameyafanya kabla ya kupambana na Yanga kisha akawapa kazi vijana wake kutafsiri ndani ya uwanja, licha ya kwamba timu hiyo ilipoteza kwa bao 1-0, lakini kimbinu kocha huyo alifanikiwa kutokana na mipango mkakati aliyoingia nao Azam Complex.


KUJENGA SAIKOLOJIA

Bila shaka hili ukiliangalia kwa umakini ndio lilikuwa suala la kwanza kufanywa kwa wachezaji, ilikuwa hakuna namna unakwenda kucheza na Yanga iliyowafunga wapinzani wako wawili waliokusumbua, wakifungwa mabao mengi .

Saikolojia ilijengwa kwa wachezaji kuingia kwenye mchezo bila kuigopa Yanga kwa maana kweli Yanga inaubora lakini ina makosa yake.

Kwamba pamoja na uchezaji wa Yanga kuwa wa kasi na pasi nyingi bado Yanga nayo ina haraka ya kuucheza mpira ili kufika golini hivyo kuwafanya wacheze kwa umakini sana.


KAZE HAKUISHIA HAPO

Ilikuwa ni mechi ngumu kwa Kaze, hivyo ulazima wa kukesha kuusoma mchezo wa Yanga ukiwa  huchezi, huku ukiangalia wapinzani wanaofuata kiufundi kocha huyo aliamua kutambulisha yafuatayo:


MFumo Mama:

Aliingia na mfumo wa kuzuia kwanza kisha kushambulia kwa kushtukiza ndani ya 5 : 3 : 2

Akiwatumia Hashim Manyanya, Charles Edward, Emmanuel Asante, Derick Mukombozi na Erasto Nyoni

Wanapopata mpira wanapanda na kuzuia kwa akili ndani ya mpango kazi wa 3 : 3 : 3 :1 hapo utawaona Erasto na Manyanya wanaondoka taratibu kuingia zone ya mbele kwa umakini mkubwa.


KUSHAMBULIA KWA KUSHTUKIZA

Ilikuwa ni rahisi kushambulia kwa kushtukiza hasa kutokana na timu yote ya Namungo kurudi nyuma kukaba kwenye zuio la chini kabisa, hii iliwafanya Yanga kushambulia karibia wachezaji wote huku kukiwa na nafasi kubwa kati ya kipa Diarra Djigui na mabeki wa timu hiyo.

Kaze alimtumia Pius Buswita na Ibrahim Abdalah kufanya mashambulizi hayo ya kushtukiza, lakini bahati mbaya wachezaji hao hawakuwa na kasi kubwa sana, pia, hawakuwa wanapeleka pasi pembeni hali ambayo ingewafanya kufanya mikimbio bora.


KUJAZA MASTAA WA TABIA MOJA

Kocha Kaze alijua njia pekee ya kuwashika wachezaji wa Yanga kwa sasa ni kutowapa nafasi ya kucheza kabisa katikati ya uwanja hivyo akamuua kuwachezesha hawa:

Nyoni, Manyanya, Jacob Massawe, Frank Domayo na Buswita ambao kazi yao ilikuwa ni kuwazuia kina Stephane Aziz KI, Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli na Khalid Aucho kitu ambacho kiliwasaidia sana.

Ukabaji wao ulikuwa kwenye umbo la 3:2 VS 2, 4 : 1 vs 3 na mara nyingi kwenye eneo lao wakiwa 6: 3: 1 hapo unaona timu nzima ikiwa imeshuka chini na kumuacha mchezaji mmoja tu juu tena kwenye nusu ya eneo lao.


GAMONDI ALITOA KILA KITU

Kwa mara ya kwanza unaona kocha wa Yanga anawaanzisha wachezaji wake watatu ambao wanaweza kucheza kwenye namba 10 na kukupa kitu kilicho bora ndani ya uwanja.

Aziz KI, Maxi na Pacome hawa wote waliamua kucheza kwa uhuru mkubwa na kuwafanya Clement Mzize na Kennedy Musonda kubaki kwenye eneo la juu ili kuwasumbua mabeki wa Namungo.

Gamondi aliwafanya wachezaji wengi kucheza ndani zaidi ili kuwapa nafasi mabeki wa pembeni Kouassi Yao na Joyce Lomalisa ambapo kama kawaida kulia ndiko kulikuwa na hatari ya kuzalisha krosi nyingi na bao pia.


KUPOTEZA PASI NYINGI

Ilikuwa siyo kawaida tangu nimeanza kuwaona Yanga kwenye msimu huu wachezaji wake wakipoteza mipira mingi ama kunyang’anywa au pasi zao kuzuiwa.

Kouassi Yao: Alipoteza pasi mbili na kunyang’anywa mpira mguuni mara moja.

Maxi Nzengeli : Pasi mbili kunyang’anywa mara mbili, kuchelewa kuufikia mpira mara moja.

Aziz KI : alipoteza mipira mara mitatu , kunyang’anywa mara moja

Kwa ujumla Yanga ilipoteza mipira zaidi ya 40, Ilipiga pasi chache kulinganisha na michezo mingi si zaidi ya 400.


UMAKINI MDOGO

Hata kama Namungo ilicheza muda mrefu ikizuia bado ilipata nafasi mbili za wazi kufunga bao, huku ikilenga lango mara tano na kupiga nje mara nne.

Yanga: Ikikosa nafasi nane, ikipiga nje ya lango mara 11, pia ilifanya pupa kutaka kufunga mara tatu. Hiyo yote ilikuwa ni kukosa umakini na kadiri muda ulivyokuwa unakwenda wachezaji wa Yanga walikuwa wakipoteza umakini.


MWAMUZI ALIKOSA UJASIRI.

Bado kuna ombwe kubwa la kukosa ubora hasa kwa waamuzi waliosimamishwa na kuondolewa kwenye kuchezesha msimu uliopita na sasa wamerudi.

Emmanuel Mwandembwa, Elly Sasii na wengine wengi wameathirika sana na kukaa nje bila kuchezesha, lakini bado wengi wanaonekana kutobadilika kiuchezeshaji .

Mwandembwa aliyekuwa kati juzi, hakuwa na ujasiri katika kutoa maamuzi kwani, kulikuwa matukio mabaya ya matumizi ya rafu hatarishi, wachezaji kuchelewesha mipira kuanzishwa, matumizi ya nguvu katika kunyang’anyana mpira miguuni na yeye ama kupuliza filimbi bila sababu . Kuna hali bora naiona kwa waamuzi wanakuja na kuchipukia na jinsi wanavyochezesha mechi kadhaa huku wakiruhusu nguvu kutumika na siyo rafu. Kaze ametupa fundisho namna ya kuwathibiti hawa wakubwa wawili, lakini isiishie hapa bali hata kwa timu zenye levo sawa nao wanatakiwa wakaze kuanzia sasa kabla ligi haijachanganya.