Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaseja, Mgosi waitwa timu ya Taifa

Muktasari:

Miongoni mwa wachezaji walioitwa katika kikosi hiko ni kipa Juma Kaseja ambaye kwa sasa anacheza Ligi Kuu katika klabu ya KMC.
Mwingine ni Mussa Mgosi ambaye ni kocha wa timu ya vijana ya Simba na wengine ni  Ibrahim Abdallah, Ahmed Juma.

Kocha wa kikosi cha timu ya Taifa ya bechi soka Boniface Pawasa ameita wachezaji 18 ambao watajiandaa kufuzu AFCON.
Miongoni mwa wachezaji walioitwa katika kikosi hiko ni kipa Juma Kaseja ambaye kwa sasa anacheza Ligi Kuu katika klabu ya KMC.
Mwingine ni Mussa Mgosi ambaye ni kocha wa timu ya vijana ya Simba na wengine ni  Ibrahim Abdallah, Ahmed Juma.
Roland Musonjo wa Mbao, Samwel Salonge, Yahya Tumbo, Jaruph Juma, Ahmada Ahmada, Soud Ame, Alfa Tindise, Kashiru Salum, Ali Badru.
Wengine Mohamed Makame, Shafii Mussa, Justine Anthony na Self Mwinyi.
Pawasa alisema kikosi hiko kitaanza mazoezi Jumamosi katika viwanja  vya fukwe ya Coco Beach.
"Nafahamu kuna kuna wachezaji ambao wapo katika majukumu ya klabu zao lakini linapofika suala la Utaifa ni muhimu kuliweka mbele na kama udhuru tutatoa katika wiki moja ya mwanzo kabla timu kuingia kambini na baada ya hapo hatutataka kuona mchezaji anakosekana," alisema Pawasa.
Kikosi hiko kitakuwa na benchi la ufundi ambalo litaongozwa na Pawasa msaidizi wake Adam Katwila, Deo Lucas atakuwa Meneja na Frank Mutago mtunza vifaa.