Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kanoute wa Simba kujiunga na Azam FC

KANOUTE Pict

Muktasari:

  • Kanaute, raia wa Mali aliondoka nchini akiwa Simba baada ya kuhudumu kwa miaka mitatu tangu msimu wa 2021-22 akitokea Al ahly Benghazi ya Libya ambapo punde tu baada ya kusajili alifanikiwa kupata namba kikosi cha kwanza mara kwa mara.

ALIYEKUWA kiungo wa Simba, Sadio Kanoute anatarajia kuwasili nchini kesho alfajiri kwa ajili ya kujiunga na Azam FC.

Kanaute, raia wa Mali aliondoka nchini akiwa Simba baada ya kuhudumu kwa miaka mitatu tangu msimu wa 2021-22 akitokea Al ahly Benghazi ya Libya ambapo punde tu baada ya kusajili alifanikiwa kupata namba kikosi cha kwanza mara kwa mara.

Baada ya kutajwa sana kuwa atajiunga na Azam FC, Mkuu wa Idara ya Habari, Thabit Zakaria 'Zaka Zakazi' amethibitisha kuwa Kanoute anatarajiwa kuwasili saa tisa alfajiri.

“Kanoute anatarajia kutua nchini alfajiri ya kuamkia kesho saa 9:00 alfajiri,” ni sehemu ya maneno machache ya Zaka Zakazi.

Ujio wa Kanoute ndani ya Azam FC kwenye eneo la kiungo mkabaji kutamfanya mchezaji huyo aungane na mkongwe Himid Mao ambaye pia ametua katika dirisha hili la usajili.

Eneo hilo pia lina Sospeter Bajana, Adolph Mtasingwa, Yahya Zayd na Ever Meza.