Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yakoleza mbio za ubingwa, Yanga ikiongezewa presha

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam, huku ikitawaliwa na ushindani wa hali ya juu, shujaa wa Simba aliyekoleza vita ya ubingwa alikuwa ni Libasse Gueye aliyefunga bao la pili dakika ya 64.

USHINDI wa Simba wa mabao 2-1, dhidi ya Pamba Jiji umezidi kuongeza presha ya mbio za ubingwa msimu huu na watani zake wa jadi Yanga, kufanya tofauti ya pointi kuendelea kubakia mbili, huku ikiwa imebakia mechi nne za kumaliza msimu wa 2025-2026.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam, huku ikitawaliwa na ushindani wa hali ya juu, shujaa wa Simba aliyekoleza vita ya ubingwa alikuwa ni Libasse Gueye aliyefunga bao la pili dakika ya 64.

Bao hilo alilofunga nyota huyo kwa ustadi mzuri baada ya kupiga mpira uliomzidi ujanja kipa wa Pamba, Yona Amos, ndilo lililoibua matumaini ya kuendelea kubakia nafasi ya pili na pointi 61, nyuma ya vinara Yanga inayoongoza na pointi 63.

Katika mechi hiyo, Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao la dakika ya saba kupitia kwa Elie Mpanzu aliyemaliza mpira wa adhabu uliopigwa na Neo Maema, kabla ya Mkenya Mathew Tegisi kuwasawazishia Pamba Jiji dakika ya 18, akimaliza vizuri mpira uliopigwa na Zabona Mayombya.

Ushindi huo kwa Simba unakuwa ni wa kwanza msimu huu dhidi ya Pamba Jiji, baada ya mechi ya kwanza iliyokuwa pia ya vuta nikuvute iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1, Machi 19, 2026.

Licha ya ushindani wa kuwania ubingwa msimu huu, ila Simba kwa sasa imefikisha jumla ya mechi 21, za Ligi Kuu Bara bila ya kupoteza, tangu walipochapwa mabao 2-0, na Azam FC, Desemba 7, 2025.

Mechi hiyo ya Desemba 7, 2025, ndiyo iliyokuwa ya mwisho kwa Simba kupoteza katika Ligi Kuu, ambapo hadi sasa imecheza 21, huku kati ya hizo ikishinda 14 na kutoka sare saba, ikiendelea kutengeneza rekodi ya kuvutia chini ya Kocha, Steve Barker.

Kwa upande wa Pamba Jiji katika mechi 26 ilizocheza hadi sasa msimu huu, imeshinda nane, sare tisa na kupoteza pia tisa, ambapo kikosi hicho cha 'TP Lindanda' au 'Wanakawekamo', kinashika nafasi ya saba, baada ya kukusanya ya pointi zake 33.

PRISONS YALIPA KISASI

Katika mechi nyingine iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini, Mbeya, wenyeji Tanzania Prisons inayopigania nafasi ya kuepuka janga la kushuka daraja ililipiza kisasa, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, dhidi ya Dodoma Jiji.

Mabao ya wenyeji Tanzania Prisons, yalifungwa na Heritier Lulihoshi aliyewahi kuitumikia Dodoma Jiji kwa penalti dakika ya nne, huku mengine yakifungwa na Oscar Mwajanga dakika ya 13 na mshambuliaji nyota wa timu hiyo, Jeremiah Juma dakika ya 66.

Bao pekee la Dodoma Jiji la kufutia machozi lilifungwa na mshambuliaji nyota wa timu hiyo, Waziri Junior dakika ya 43, ikiwa ni kisasi kwa Prisons, baada ya mechi ya raundi ya kwanza iliyopigwa Januari 22, 2026, kukubali kichapo cha bao 1-0.

Licha ya Prisons kuibuka na ushindi huo, inaendelea kubakia nafasi ya 15 na pointi 23, baada ya kushinda mechi sita, sare tano na kupoteza 15, huku Dodoma Jiji ikiwa ya nane na pointi 33, ikishinda nane, sare tisa na kupoteza pia tisa.