Kahama Sixers, Risasi vita nzito Shinyanga

Muktasari:
- Katika fainali ya mwaka jana, Kahama Sixers iliishinda Risasi michezo 2-1 na katika mchezo wa kwanza ilishinda pointi 67-62. mchezo wa pili, Risasi ilishinda kwa pointi 102-100, huku Kahama Sixers ikishinda katika mchezo wa tatu kwa pointi 87-60.
Kahama Sixers na Risasi zinatarajiwa kucheza Jumapili mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Mkoa wa Shinyanga.
Katika fainali ya mwaka jana, Kahama Sixers iliishinda Risasi michezo 2-1 na katika mchezo wa kwanza ilishinda pointi 67-62. mchezo wa pili, Risasi ilishinda kwa pointi 102-100, huku Kahama Sixers ikishinda katika mchezo wa tatu kwa pointi 87-60.
Kamishina wa ufundi na mashindano wa ligi ya kikapu wa mkoa wa huo, George Simba alisema mchezo huo wa ufunguzi utachezwa katika Uwanja wa Kahama.
Alizitaja timu zitakazoshiriki ligi hiyo mwaka huu ni B4 Mwadui, Risasi, Kahama Sixers na Veta.
Simba alisema mfumo utakaotumika ni wa kila timu kucheza nyumbani na ugenini na timu itakayoshika nafasi ya kwanza itacheza na ya nne, ya pili na ya tatu na kila timu itacheza michezo mitatu ‘best of three play off’.