Jose Mourinho akanusha mpango wa kumhitaji Bale msimu huu

Muktasari:

  • Mourinho amesisitiza kwamba mpago wake msimu huu ni kuhakikisha mlinda mlango wake, David De Gea anaendelea kubaki kwenye dimba la Old Trafford.

London, England. Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema hajafanya mazungumzo na Real Madrid wala kuwa na mpango wa kumsajili Gareth Bale.

Mourinho amesisitiza kwamba mpago wake msimu huu ni kuhakikisha mlinda mlango wake, David De Gea anaendelea kubaki kwenye dimba la Old Trafford.

Awali, kulikuwa na taarifa kuwa Mashetani Wekundu hao walikuwa kwenye mkakati wa kumsajili mshambuliaji huyo aliyewahi kuweka rekaodi ya usajili.