Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKU yautaka ubingwa ZPL

MAAFANDE wa JKU wameendelea kuwa wababe wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) baada ya kuwa na kujikusanyia pointi tatu nyingine kwenye mechi zao.

Hivi karibuni iliifunga Kipanga FC bao 1-0 na kuendelea kuongoza ligi hiyo kwa pointi 29 wakiwazidi Zimamoto na KVZ wenye pointi 23 kila mmoja na kabla ya michezo ya jana.

JKU imekuwa na kiwango kizuri msimu huu na mashabiki wengi wanaipa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kama wataendelea na kasi hii.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha mkuu wa JKU, Salum Ali Haji alisema kwa sasa hawezi kujisifia kama wapo vizuri lakini anaamini timu yao ni bora ndio maana wanaongoza ligi.

Alisema hawana asilimia 100 ya kutwaa ubingwa kwa sababu mechi zilizobaki ni nyingi kuliko walizocheza lakini dhamira yao ni  kuchukua ubingwa msimu huu.

“Sasa hivi bado mapema sana kutangaza ubingwa, lakini ni dhamira yetu ndio maana kila mechi tunakuwa na mbinu mpya na kila mechi kwetu ni fainali, tumebakiwa na michezo 18 kukamilisha msimu mzima lolote linaweza kutokea,” alisema.

JKU ndiyo timu pekee iliyopoteza mchezo mmoja tu hadi sasa wakicheza mechi 12, sare mbili na kushinda michezo tisa, mwezi ujao Desemba 2 watashuka uwanja wa Mao Zedong A kucheza dhidi ya Malindi, mechi itakayoanza saa 10:15 jioni.