Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT, Kagera zavuka maji kumsaka Pina

Muktasari:

  • Timu hizo ni JKT Tanzania pamoja na Kagera Sugar iliyorejea Ligi Kuu Bara, huku zote zikiwa katika hatua nzuri ya mazungumzo na Pina.

TAARIFA kutokea visiwani hapa zinabainisha kwamba, kuna timu mbili kutokea Tanzania Bara, zimevuka maji kumfuata mshambuliaji Abdallah Iddi 'Pina' kwa ajili ya kutaka huduma yake kuelekea msimu ujao.

Timu hizo ni JKT Tanzania pamoja na Kagera Sugar iliyorejea Ligi Kuu Bara, huku zote zikiwa katika hatua nzuri ya mazungumzo na Pina.

Akizungumza na Mwanaspoti, mshambuliaji huyo amekiri kuwepo kwa tetesi hizo, huku akibainisha kwamba bado wapo katika mazungumzo, hivyo wakifikia muafaka ataweka wazi.

"Tupo kwenye mazungumzo bado hatujafikia muafaka, tukikubaliana kila kitu kitakuwa wazi na kila mmoja ataelewa," alisema Pina.

Alisema, kwa msimu ujao anatamani zaidi kucheza tena Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kukosa fursa hiyo msimu huu 2025-2026 licha ya kusajiliwa na Pamba Jiji.

Alieleza kuwa, baada ya kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Zanzibar msimu wa 2024-2025, alikuwa na ndoto nyingi akiamini zingeenda kutimia ndani ya Pamba Jiji iliyomsajili kipindi cha dirisha kubwa, lakini majeraha yalikatisha matumaini yake akajikuta anakaa nje hadi dirisha dogo alipoomba kutolewa kwa mkopo akiwa hajacheza mechi hata moja ya ushindani.

Hivyo, alisema msimu ujao ataonesha utofauti na misimu mingine kwa sababu amejipanga vizuri kukabiliana na ushindani utakaokuja mbele yake.

"Mkataba wangu na Pamba Jiji umebaki mwaka mmoja, lakini wameridhia nikipata timu naweza kujiunga nayo kwani hata nilipoomba kutolewa kwa mkopo kuja Muembe Makumbi, waliniruhusu vizuri kwa sababu nilikuwa na mawasiliano mazuri na viongozi wangu," alibainisha Pina.