Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jesus Moloko kuibukia Angola

MOLOKO Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyejiunga na Mbeya Kwanza katika dirisha dogo la Januari 2026, hivi karibuni aliondoka kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo mjini Tabora ikijiandaa na mechi ya Play-Off, kusaka tiketi ya kupanda Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania.

ALIYEKUWA winga wa Mbeya Kwanza iliyoshiriki Ligi ya Championship msimu wa 2025-2026, Mkongomani Jesus Ducapel Moloko, yupo katika hatua za mwisho za kujiunga na Klabu ya Primeiro de Maio inayoshiriki Ligi Kuu ya Angola maarufu Girabola.

Nyota huyo aliyejiunga na Mbeya Kwanza katika dirisha dogo la Januari 2026, hivi karibuni aliondoka kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo mjini Tabora ikijiandaa na mechi ya Play-Off, kusaka tiketi ya kupanda Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania.

Akizungumza na Mwanaspoti, Moloko amesema aliondoka katika kambi hiyo kwa ajili ya kushughulikia changamoto mbalimbali alizokuwa nazo, japo suala la kujiunga na timu nyingine akisema kwa sasa bado, licha ya kukiri mkataba wake tayari umemalizika..

MOLO 01

“Nilisaini mkataba wa miezi sita na Mbeya Kwanza na nipo huru kujiunga na timu nyingine msimu ujao, nashukuru kwa sapoti kubwa niliyoipata toka mwanzo, japo hatujaweza kufikia malengo ya kupanda Ligi Kuu Bara moja kwa moja,” amesema Moloko.

Hata hivyo, Mwanaspoti linatambua Moloko aliondoka Mbeya Kwanza kwa kile kinachodaiwa anaidai mshahara wa zaidi ya miezi mitatu, jambo lililosababisha nyota huyo kutua jijini Dar es Salaam ili kuamua mustakabali wake upya.

MOLO 02

Nyota huyo aliyewahi kuitumikia Yanga kuanzia Agosti 13, 2021 hadi Januari 28, 2024, wakati alipojiunga na kikosi hicho akitokea AS Vita ya kwao DR Congo, alijiunga na Mbeya Kwanza Januari 2026, baada ya kuachana na AS Kigali kutoka Rwanda.

Moloko alijiunga na AS Kigali Agosti 28, 2025, baada ya kuachana na ES Mostaganem ya Algeria, ingawa hakudumu nayo baada ya kuondoka Januari 2026, huku akichezea timu mbalimbali zikiwemo za Diyala SC ya Iraq na Al Sadaqa Shahat SC ya Libya.

Katika Ligi Kuu ya Angola msimu wa 2025-2026, Primeiro de Maio imemaliza nafasi ya nane na pointi 37, baada ya kushinda mechi 10, sare saba na kupoteza 13, huku ikifunga mabao 29 na kuruhusu 33.