Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Inter Zanzibar, Tekeleza zashuka rasmi ZPL

DARAJA Pict

Muktasari:

  • Timu hizo ni miiongoni mwa nne zilizopanda Ligi Kuu msimu huu, sambamba na vinara wa ligi hiyo kwa sasa, Mwembe Makumbi na Junguni United.

SAFARI ya Inter Zanzibar na Tekeleza katika Ligi Kuu ya Zanzibar (ZPL), imefikia tamati jioni leo baada kufungwa mabao 4-0 na KVZ, huku Tekeleza nayo ikishuka daraja kwa kufungwa huko Pemba.

Timu hizo ni miiongoni mwa nne zilizopanda Ligi Kuu msimu huu, sambamba na vinara wa ligi hiyo kwa sasa, Mwembe Makumbi na Junguni United.

Inter iliyovuna pointi tano kupitia mechi 23, ilikumbana na kipigo hicho kwenye Uwanja w Mao A jioni ya leo Ijumaa.

KVZ ilianza karamu ya mabao dakika ya 34 kupitia kwa Yohana Mkomola, bao lililodumu hadi mapumziko kabla ya  kupata mengine matatu kipindi cha pili.

Mabao hayo yaliwekwa wavuni na Salum dakika ya 52 na Michael Joseph aliyetupia mawili dakika ya 63 na 72.

Kutoka Uwanja wa Gombani,  Pemba,  Junguni United iliizamisha Tekeleza kwa kuifunga mabao 2-0 na kuishusha rasmi daraja. Mabao ya washindi yaliyofungwa na Abubakar Malik dakika ya 17 na Mohamed Hashim dakika ya 72. 
Matokeo hayo yameiacha Telekeza ambayo haijaonja ushindi katika ligi hiyo iliyoipanda msimu ikisalia na pointi tatu kupitia mechi 23.

Tekeleza na Inter Zanzibar zinakuwa timu mbili za kwanza kushuka na kuacha msala kwa timu nyingine mbili za kufunga hesabu nne zinazotakiwa kushuka ili kupisha za kupanda kwa msimu  ujao.