Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Inonga atibua hesabu Simba

Beki wa simba, henock inonga ametoka hospitalini baada ya kujeruhiwa kwenye mchezo wa juzi huku kocha wake akitikisa kichwa na akisema muda ambao wanaweza kumkosa.

Inonga aliumia juzi wakati simba ikiifunga coastal union ya tanga kwa mabao 3-0 ikiwa ni mechi ya ligi kuu bara, aliumia katika dakika ya 20 kipindi cha kwanza na kuwahishwa hospitalini kushonwa jeraha hilo la mguuni baada ya kukanyagwa na haji ugando. kilinda ugoko cha inonga kilivunjika.

Kocha wa simba, roberto oliveira ‘robertinho’ (63) alisema kuumia kwa beki huyo kunatibua hesabu zake ambapo taarifa ya awali ya daktari wa timu ni kwamba ameshonwa nyuzi zisizopungua 12 na wanaweza kumkosa kwa siku kati ya 15-20.

Hata hivyo, daktari wa timu hiyo, edwin kagabo alisema bado wanasubiri ripoti kamili ya vipimo vingine ili waweze kutoa ripoti ya ujumla baadaye wikiendi hii.

“Tunasubiri ripoti kamili ya vipimo vingine vya mguu wake na tutakapovipata tutatoa taarifa kamili ya muda gani atakuwa nje au utatumika kupona kwake,” alisema kagabo.

Kwa upande wa robertinho alisema; “ni habari mbaya sana kwetu hasa wakati huu tunatafuta muunganiko wa timu yetu, tupo kwenye wakati wa kuiunganisha timu na mchezaji na beki bora afrika ameumia vibaya.

“Kwa haraka haraka nadhani tunaweza kumkosa kwa siku 15 au 20, kile ni kidonda kikubwa kilichohusisha ushonaji wa nyuzi kama 12 au zaidi, itategemea atakuwa na uponaji wa haraka kwa namna ipi, tunamuombea sana apone haraka,” aliongeza.

Pia robertinho alisema tukio lile liliwaumiza wachezaji wake kwa mshtuko na kuwafanya kushindwa kujituma uwanjani mara baada ya kuona jeraha lake.

“Kuna mchezaji aliniomba nimtoe, lakini nilikataa ilihitaji kuwajenga kisaikolojia, wenzake.”