Ikobela ampisha Mwaipasi City ikivaa KMC

Saturday November 27 2021
KMC PIC
By Saddam Sadick

Mbeya. Wakati Mbeya City ikishuka dakika chache zijazo uwanjani kuwakabili KMC, Kocha mkuu wa timu hiyo, Mathias Lule amefanya mabadiliko ya mchezaji mmoja, akimpumzisha Winga Frank Ikobela aliyetumika mechi iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar na kumuanzisha Gasper Mwaipasi.

Katika mechi iliyopita Mbeya City ikiwa nyumbani iliizamisha Mtibwa Sugar mabao 3-1 na leo Jumamosi itakuwa Sokoine jijini Mbeya kuwakaribisha KMC mechi itakayopigwa saa 10:00 jioni.

Katika kikosi kilichoanza leo ni Haruon Mandanda, Keneth Kunambi, Mpoki Mwakinyuke, Samson Madeleke, Juma Shemvuni, Aziz Andabwile, Gasper Mwaipasi, Seleman Ibrahim, Paul Nonga, Juma Luizio na Richardson Ng'ondya.

Kwa upande wa KMC, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Habibu Kondo amewaanzisha, Farouk Shikhalo, Kelvin Kijiri, Ally Ramadhan, Andrew Vicent Sadalah Lipangile, Abdulrazak Hamza, Abdul Hassan, Kenny Mwambungu, Matheo Simon, Emanuel Mvuyekule, na Miraji Athuman.

Timu hizo zinakutana ikiwa kila upande unakumbuka ushindi katika mechi iliyopita, ambapo KMC waliichakaza Azam FC mabao 2-1 huku Mbeya City wakiishindilia Mtibwa Sugar mabao 3-1.

Advertisement