Ihefu yadaka kiungo wa AFCON

Muktasari:

  • Amade ni kiungo mkabaji anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Ud Songo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Msumbiji.

MABOSI wa klabu ya Ihefu hawatanii kwani wameamua kukitengeneza kikosi chao kwenye dirisha hili dogo kwa kumsajili kiungo mkabaji, Amade Momade ‘Amadou’ anayekipiga katika timu ya Taifa Msumbiji inayoshiriki Mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON) yanayoendelea nchini Ivory Coast.

Amade ni kiungo mkabaji anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Ud Songo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Msumbiji.

Kiungo huyo anayevaa jezi namba 6,  kwenye mchezo wao wa kwanza jana dhidi ya Misri uliomalizika kwa sare 2-2 aliingia dakika tisa za mwisho.

Amade awali alikuwa anahusishwa kwenda TS Galaxy lakini hata hivyo Ihefu imepindua dili hilo.

Ihefu awali ilianza kutengeneza benchi lake la ufundi kwa kumchukua Mecky Maxime na Mathias Lule na sasa imegeukia upande wa wachezaji.

Habari za uhakika ni kwamba kuna panga kubwa linapita katika kikosi cha Ihefu na kuingia maingizo mapya.

Wachezaji wanaotajwa kuingia kwenye timu hiyo ni Elvis Rupia, Kelvin Nashon. Na Joash Onyango wote kutoka kikosi cha Singida Fountain Gate.