Huyo Azizi Ki ageuka wimbo kwa Mkapa

MAVITU anayofanya Aziz Ki yanaonekana kuwakosha mashabiki wa Yanga na kuamua kuanza kuimba jina la raia huyo wa Burkina Faso.

Azizi Ki ndiye mpishi aliyepika bao la kusawazisha kwa Yanga lililofungwa na Fiston Mayele dakia ya 68 ya mchezo.

"Azizi, Azizi," waliskika mashabiki hao wa Yanga mara kwa mara wakiimba jina la staa huyo aliyesajili kutoka ASEC Mimomas ya Ivory Coast, ambapo alimaliza ligi kuu nchini humo akitwaa tuzo ya mchezaji bora.

Tangu aanze kutumika kama namba 10 katika kipindi cha pili anaonekana kuwa na madhra zaidi kwa Simba tofauti na awali ambapo alikuwa akitokea pembeni.

Katika mchezo huo wa fainali ya Ngao ya Jamii kati ya vigogo hao wa Kariakoo imetamatika kwa Yanga kuibuka kidedea kwa mara ya mpili mfululizo huku muuaji akiwa yuleyule Fiston Mayele.