Huko Yanga ni shida!

Muktasari:

Zahera mipango yangu mingi ya kuhakikisha Yanga inakuwa bora naona kabisa inakwama kutokana na ukata unaoikabili viongozi nashindwa kufanya uamuzi kwa kusubiri nini watakifanya dirisha dogo la usajili.

KWA hali halisi inayoendelea ndani ya kikosi cha Yanga ni dhahiri inaweza  kukwamisha mpango ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera ya kutaka kuwatema baadhi ya nyota ambao hakutaka kuendelea nao mzunguko wa pili.
Zahera aliliambia Mwanaspoti kwamba anashindwa kufanya maamuzi kwa sasa ya kuwatoa kwa mkopo wachezaji ambao hawakuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho kutokana na hali ya ukata uliopo ndani ya timu.
Alitoa sababu ya kauli yake kwamba anaona hali ya kiuchumi bado haijatengemaa ndani ya timu hiyo  na kupelekea kuwa na wasiwasi wa kuona mipango yake kabambe ya kutema na kusajili wachezaji inaweza isifike mwisho ingawa alikiri muda bado, lakini kujihami ndio akili.
"Kwa sasa nitatawaliwa na kimya cha wachezaji gani ninaweza nikawaacha kwani ngumu kuwatema kama itakosekana pesa ya kuwaleta wale ambao wataziba mapengo yao kupitia usajili wa dirisha dogo.
"Nilifanya zoezi la kuwapatia viongozi wangu majina ya wachezaji ninaowahitaji na wanaotakiwa kuachwa , siwezi kuwalazimisha angali najua hali halisi ya timu ilivyo kwasasa, naamini wanapambana ndio maana naendelea kusubiri,"alisema Zahera.
Nje na hilo pia alisema mashabiki wa Tanzania wajifunze kujitoa kwa hali na mali kwa klabu zao wanazozipenda kuliko kutoa kasoro ambazo hawajua nini kinawakabili wachezaji nje ya uwanja.
"Natamani kuwa na mchezo wa kirafiki kabla ya ligi aijaanza kupisha timu yao ya Taifa Taifa Stars lengo ni kujaribu kuwaweka karibu wachezaji wangu na mashabiki zao waweze kujua kuwa wachezaji wanakabiliwa na changamoto nyingi sana mimi napambana kuwatuliza na ndio maana timu inapata matokeo," alisema
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussein Nyika ili kuzungumzia changamoto hiyo alisema muda wa kufunguliwa kwa dirisha la usajili bado haujafika ukifika watafanya kama walivyoagizwa na kocha wao.
"Dirisha la usajili bado halijafunguliwa kwasasa tuko bize kuiandaa timu iweze kupata matokeo mazuri michezo yake yote iliyobaki muda wa usajili ukifika tutasajili kama maelekezo ya mwalimu yalivyo kuhusu ukata katika timu hiyo ni ishu nyingine baina ya timu na viongozi hatuwezi tukakwambia sasa tuna pesa au hatuna," alisema Nyika.