Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hivi ndivyo vyakula pendwa Morocco

Muktasari:

  • Kama ilivyo kwa jamii ya Kihaya ambayo ndizi zilizochanganywa na maharage ndiyo chakula kinachoitambulisha, kwa hapa Morocco vipo vyakula viwili ambavyo vinapendwa kwa kiasi kikubwa na jamii ya yao.

Berkane: KILA nchi ina utamaduni wake na vyakula, kuna wakati huwa ni utambulisho wa nchi au jamii fulani.

Kama ilivyo kwa jamii ya Kihaya ambayo ndizi zilizochanganywa na maharage ndiyo chakula kinachoitambulisha, kwa hapa Morocco vipo vyakula viwili ambavyo vinapendwa kwa kiasi kikubwa na jamii ya yao.

Vyakula hivyo viwili vya kitamaduni vya Morocco ni Tajini na Kusi Kusi ambavyo huwa na staili tofauti za kupikwa kwake.

Chakula cha Tajini ni kama supu fulani hivi au urojo kama ilivyo kwa nyumbani Tanzania ambacho ndani yake huwa na nyama, mayai ya kuchemsha, viazi na zabibu kavu.

Viungo vinavyotumika katika mapishi ya Tajini ni nyanya, bizari, tangawizi, vitunguu saum, vitunguu maji, pilipili na iriki ambavyo husagwa pamoja na kuchanganywa katika mchuzi wa kupikia chakula hicho.

Kwa upande wa chakula cha Kusi Kusi, kinapikwa kwa kuchanganya wali, kuku, nyama ya ng’ombe au kondoo, pilipili hoho, bilinganya, karoti na nyanya chungu.

Kwa maana ya gharama, chakula kinachouzwa kwa bei kubwa zaidi ni Tajini ambapo ni kama Sh50,000 fedha za Kitanzania na Kusi Kusi ni kama Sh30,000.