Helmy Gueldich atua Orlando Opirates

KOCHA wa viungo wa zamani wa klabu Yanga, Helmy Gueldich rasmi amejiunga na timu ya Orlando Pirates kuitumikia kwa msimu mpya baada ya kumalizana na kikosi hicho.
Helmy raia wa Tunisia, aliitumikia Yanga miaka miwili na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo akiwa miongoni mwa benchi la ufundi chini ya aliyekuwa Kocha Nasredine Nabi.
Kocha huyo mwenye ujuzi wa takribani miaka minne (4), katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Mazoezi nchini Tunisia na kufanikiwa kupata elimu ya viungo na utendaji wa michezo.
Safari yake ya soka ilianzia katika klabu ya CS Sfavien ya Tunisia ambapo alikuwa mchezaji wa timu hiyo kubwa na kongwe walikuwa mabingwa wa Kombe la Shirikisho CAF-2007, 2008 na 2013.
Orlande Pirates imemtambulisha rasmi kocha huyo wa viungo kuwa miongoni wa benchi la ufundi litakalo ongozwa na Kocha Jose Riveiro, wakifatiwa na wasaidizi Mandla Ncikazi na Sergio Almenara, pamoja na mkufunzi wa makipa Tyron Damons.