Hatma ya kina Mayay, Dk Msolla kujulikana leo

Muktasari:
- Wagombea sita wa nafasi ya Urais akiwamo anayetetea kiti, Wallace Karia, Ally Mayay, Dk Mshindo Msolla, Injinia Mustapha Himba, Ally Mbingo na Shija Richard, pamoja na wengine 19 wanaowania nafasi sita za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo wamejitosa katika uchaguzi huo.
MCHAKATO wa Uchaguzi Mkuu wa TFF unaendelea kwa leo kuingia hatua ya usaili ambapo hatma ya wagombea 25 waliojitokeza kuchukua na kurudisha fomu inatarajiwa kufahamika baada usaili huo ulioanza tangu asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam.
Wagombea sita wa nafasi ya Urais akiwamo anayetetea kiti, Wallace Karia, Ally Mayay, Dk Mshindo Msolla, Injinia Mustapha Himba, Ally Mbingo na Shija Richard, pamoja na wengine 19 wanaowania nafasi sita za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo wamejitosa katika uchaguzi huo.
Usahili wa wagombea hao unaoendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), umeanza tangu saa 4:00 asubuhi ya leo ukianza na wagombea na nafasi ya Urais ukifanyika kwenye Hoteli ya Tiffany.
Tayari Dk Mshindo Msolla amekuwa wa kwanza kumaliza kufanyiwa usahili na kuondoka hotelini hapo akiambatana na mwanaye Mbete Msolla
Wagombea wengine wanaosubiriwa kutoka ni Ally Mayay, Injinia Mustapha Himba, Ally Mbingo,Shija Richard na rais anayetetea kiti hicho Wallace Karia.
Baada ya wagombea hao kumaliza usahili huo watafuata wajumbe wanaowania nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji waliopo19, watakaoanza usaili huo saa 8 mchana kisha watakaopenya watafahamika kabla ya kuendelea na mchakato wa uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 16, jijini Tanga.