Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola kupewa Alaba, hela amtoe Leroy Sane

MUNICH, UJERUMANI. MANCHESTER City wametengewa ofa ya kumchukua kiraka David Alaba pamoja na pesa juu ili wamwachie winga wao moto wa Kijerumani, Leroy Sane kwenda kujiunga na Bayern Munich katika dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.
Alaba, ambaye mwenye uwezo wa kucheza beki ya kushoto na kiungo wa kati amekuwa mchezaji staa huko kwenye Bundesliga, lakini taarifa zinadai kwamba yupo tayari kwenda kukabiliana na changamoto mpya kwingineko.
Bayern Munich kwa muda mrefu wamekuwa wakihitaji saini ya Sane nna mwaka jana walishindwa kunasa saini yake baada ya mchezaji huyo kuumia. Na sasa wasiwasi wao ni kwamba wanaamini klabu nyingine nyingi zitahitaji huduma ya mchezaji huyo wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa.
Kocha wa Man City, Pep Guardiola atavutiwa na mpango wa kumchukua Alaba baada ya wawili hao kuwa na uhusiano mzuri walipokuwa pamoja huko Allianz Arena. Bayern ukimweka kando Alaba, wataweka mezani pia mkwanja wa Pauni 50 milioni.
Lakini, taarifa ya kutoka Etihad ilifichua: “Leroy hauzwi, lakini kumekuwa na klabu nyingi zinazohitaji saini yake.
“Inafahamika wazi kwamba Pep na Alaba wamekuwa na uhusiano mzuri baada ya kumfanya kuwa staa mkubwa huko nyuma. Lakini, thamani ya Leroy itabaki palepale. Lazima kuwe na pesa ya kutosha kukamilisha dili lake.”
Man City wanamthaminisha Sane kuwa na thamani ya Paunni 130 milioni na watakuwa tayari kumruhusu aondoke kama tu Bayern Munich watakuja na mkwanja huo.