Gor Mahia, safari ya kwenda Lusaka kizungumkuti

Nairobi, Kenya. UNAPOSOMA taarifa hii, mchana wa leo Jumapili Februari 21, 2020, mabingwa wa soka nchini, Gor Mahia bado hawajaondoka nchini kuelekea Lusaka, kwa ajili ya mechi ya marudiano ya kombe la Shirikisho la Afrika.

KOgalo walitarajiwa kuelekea Zambia, siku ya ijumaa, kwa ajili ya mechi ya marudiano, baada ya kuandikwa 1-0 na Napsa Stars, wikendi iliyopita. Baadae ikadaiwa kuwa, mlezi wao, Raila Odinga, ameingia kati na kwamba, wangeondoka Jumamosi (jana).

Hata hivyo, hilo nalo halikutokea, maana yake ni kwamba, safari ikawa imeahirishwa hadi Jumapili (leo) asubuhi, ambapo walipaswa kuondoka nchini saa 11 asubuhi, kwa ajili ya mechi hiyo, ambayo itapigwa leo saa 10 alasiri. Hilo nalo halikutokea.

Kwa mujibu wa habari za uhakika, zilizofika katika meza ya Mwanaspoti ni kwamba, hadi kumfikia sasa, Carlos Manuel Vaz Pinto na vijana wake, bado wameonekana katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA), huku dalili za kuondoka zikiwa hazipo kabisa.

HII INAMAANISHA NINI?

Hii inamaanisha kuwa, kwa vyovyote vile ni ngumu kwa Gor Mahia, ambao wanahitaji ushindi, kufuzu hatua inayofuata, baada ya kufungwa nyumbani, haiwezi kutua Lusaka, ikiwa katika hali nzuri ya kukabiliana na mechi ya saa 10 alasiri. Hawatokua na muda wa kupumzika au kuzoea nyasi za uwanja wa ugenini.

Kutoka Nairobi hadi Lusaka kwa Ndege, inawakosti Kogalo sio chini ya masaa mawili. Kutoka uwanja wa ndege hadi Uwanjani pia sio chini ya lisaa limoja. Kwa hiyo hadi wa nafika uwanjani, watatumia. Zaidi ya masaa matatu. Hiyo ni saa 8:30 mchana.

Bado kuna kupumzika na kula chakula cha mchana na kupumzika tena. Hapo kwa haraka wanahitaji sio chini ya saa moja. Hiyo ni saa 9:30 alasiri. Kwa maana kuwa, ukiachana na swala la kupima Afya, mambo ya Corona, ili wawe fiti kuingia uwanjani, Maandalizi ya haraka watamaliza 9:30 alasiri.

KWANINI HAWAKUSAFIRI IJUMAA?

Kwa mujibu wa viongozi wa Gor, ambaye hakutaka Jina lake kutajwa, Shirikisho la soka nchini (FKF), ndio ya kulaumiwa, kuhusu sababu za kwanini Gor ilishindwa kusafiri siku ya ijumaa. Inadaiwa kuwa, FKF ilikuwa imeahidi kugharamia tiketi za safari, lakini baadae ikasema kuwa haiwezi kusaidia klabu hiyo.

“Tuliahidiwa na FKF, kuwa tutapatiwa tiketi za ndege, lakini ilipofika Ijumaa, FKF hiyo ilituambia kuwa hawawezi kugharamia tiketi kama walivyoahidi hapo awali, kwa sababu a kaunti zao, zilikuwa zimefungiwa na KRA, katika hali hiyo, Gor Mahia, ilijikuta ikiwa haina jinsi tena," alisema Kiongozi huyo.

Alipoulizwa kuhusu ukweli wa madai hayo, Mkurugenzi mkuu wa FKF, Barry Otieno, alithibitisha na kukiri kuwa, FKF ilikuwa imejipanga kusaidia Gor Mahia, kupata tiketi za Ndege, lakini kutoka na tatizo hilo la akaunti zao kufungwa na KRA, wasingeweza kufanya hivyo tena.


Imeandikwa na FADHILI ATHUMANI