Gomes: Tunaenda kuendeleza tulipoishia

Tuesday April 06 2021
New Content Item (2)
By Thomas Ng'itu

KOCHA mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Al Ahly, wanaendeleza pale walipoishia.

Akizungumza na Mwanaspoti akiwa katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Terminal 3 Dar es Salaam, Gomes amesema mchezo huo wanaupa kipaumbele licha ya kuwa wameshafuzu.

kuondoka pic

“Tulikuwa na lengo la kumaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi na tumefanikiwa, tunaenda katika mchezo huu tukiwa vizuri na kuendelea kupambana”.

Gomes amesema wanataka kuwa katika kiwango kilekile cha ubora licha ya kukiri mchezo utakuwa mgumu.

kuspa pic
Advertisement

“Mwezi mmoja uliopita tulikuwa na mchezo mgumu dhidi yao hapa nyumbani, tukiwa ugenini tunajua tutakutana na ugumu mwingine lakini tutapambana”.

Simba wanaingia katika mchezo huo wakiwa na rekodi ya kuifunga Al Ahly 1-0 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Advertisement