Gomes: Simba bora inakuja

Tuesday September 21 2021
gomes pic
By Thobias Sebastian

KOCHA wa Simba, Didier Gomes amesema kikosi chake kimecheza vizuri katika mbinu na mahitaji mbalimbali ambayo waliyafanyia kazi kwenye maandalizi, lakini walishindwa kufunga mabao tu dhidi ya TP Mazembe.

Gomes alisema: “Nina imani kubwa na kikosi changu wale wachezaji wapya na waliokuwapo katika kikosi msimu uliopita watarudi kwa kiwango bora zaidi katika mechi ya Yanga ambayo nina imani tutaanza msimu vizuri kwa kushinda taji.

“Tumefanya maandalizi ya kutosha wakati huu ni jinsi gani tunafanya mazoezi ya mbinu - kwa maana ya kurekebisha makosa machache na kuboresha maeneo tuliyokuwa bora ili kuhakikisha tunaanza msimu kwa kuchukua taji kama tulivyomaliza msimu kwa kushinda taji.

“Umakini mkubwa tutaendelea kuwa nao kama kufanya awamu moja ya kuangalia video ya ambavyo wapinzani wetu wamecheza msimu huu na kuona mambo mengi kutoka kwao ambayo tutayatumia.”

Katika hatua nyingine Gomes alisema kwa siku zilizobaki wanaendelea kufanya maandalizi ya kutosha ili kucheza kwa usahihi zaidi ya mchezo wa TP Mazembe na kuanza msimu vizuri kwa kuchukua ubingwa wa kwanza mapema.

“Mashabiki wa Simba wanatamani kuona jambo hilo la kupata ushindi linawezekana ili furaha yao waliamaliza nayo msimu waendelee nayo, tupo tayari kupigana kwa ajili yao ili kufanikisha hili.”

Advertisement
Advertisement