Giroud ataiaga rasmi chelsea mwezi Januari

Thursday October 08 2020
giround pic

 STRAIKA wa Chelsea, Olivier Giroud yupo kwenye hatihati ya kuondoka katika dirisha lijalo la usajili majira ya baridi baada ya nafasi yake kikosi kwanza kuwa finyu.

Giroud, 34, amekuwa anawindwa na Inter Milan ambayo inafundishwa na Antonio Conte ambaye aliwahi kumfundisha akiwa Chelsea, hivyo anamhitaji akiamini anaweza kucheza kulingana na mifumo yake.

Mbali ya Inter, Juventus pia ipo kwenye harakati za kuwania saini na Chelsea ipo tayari kusikiliza ofa kutoka klabu yoyote kwa kuwa umri wa mchezaji huyo umeenda sana na kocha Frank Lampard anataka kutengeneza timu kupitia vijana. Mkataba wa mchezaji huyo unatarajiwa kumalizika 2021 huku thamani yake katika soko la usajili ni Euro 7 milioni.

 

Advertisement