Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gift Macha aula soka la ufukweni

Muktasari:

Gift Macha aliwahi kuwa mwandishi wa habari za michezo wa Mwananchi Communications lakini pia amewahi kuwa Ofisa Habari wa Mashindano ya soka la Ufukweni ya Copa Dar es Salaam yaliyofanyika mwaka 2019 jijini Dar es Salaam

MWANDISHI wa habari wa zamani wa gazeti la Mwanaspoti, Gift Macha ameteuliwa kuingia katika Kamati ya Habari na Mawasiliano ya Chama cha Soka la Ufukweni Afrika (ABSU), uteuzi uliofanyika jana Jumatano.

Taarifa iliyotolewa na ABSU jana, imeeleza kwamba Macha ambaye amewahi kuwa Ofisa Habari wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 20 'Ngorongoro Heroes' ni miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo mpya yenye wajumbe saba kutoka nchi mbalimbali.

Katika kamati hiyo ambayo Macha ameteuliwa kuwemo, mwenyekiti atakuwa ni Yaw Ankrah  kutoka Ghana huku Makamu Mwenyekiti atakuwa ni Ayo Ibidapo kutoka Nigeria na wajumbe wengine watakuwa ni Marieme Ndiaye (Senegal), Aisha Kuta (Nigeria), Nasil Auwal (Nigeria) pamoja na Namhla Mphelo (Afrika Kusini)

Ukiondoa Macha, Watanzania wengine wawili wameteuliwa kuingia katika kamati za chama hicho beki wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa ni Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, Boniface Pawasa, ameteuliwa kuingia kamati ya Ufundi wakati Jonathan Kasano ameteuliwa kuuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoonekana kupiga hatua katika soka la ufukweni ambapo imewahi kushirki fainali za Afrika za mashindano hayo mwaka 2018 na kuishia hatua za awali.