Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Geita, Namungo kazi ipo Nyankumbu

GEITA Gold imenogewa baada ya katikati ya wiki kupata ushindi wa bao 1-0 nyumbani dhidi ya JKT Tanzania, wametamba na leo wanataka tena wakati wakatapoikaribisha Namungo kwenye mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Shule ya Nyankumbu, mjini Geita.

Timu hizo zitavaana kuanzia saa 8 mchana, ikiwa ni moja ya mechi zinazochezwa leo ikiwamo ile ya JKT Tanzania itakayovaana na Ihefu kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam, huku zote zikitokea kuchezea vichapo mbele ya Geita na Namungo kwenye michezo iliyopita.

Geita ambayo kwenye mechi 10 imeshinda mbili tu, ukiwamo uliopita, imesema inataka kutumia mechi hiyo ya nyumbani ili kuongeza pointi licha ya kukiri ni mchezo mgumu, kwani Namungo ipo vizuri.

Kocha Msaidizi wa Geita, Choki Abeid, alisema; “Tumeiandaa timu yetu tukijua tuna mchezo mgumu dhidi ya Namungo ambayo iko kwenye kiwango chake kizuri, lakini kama unavyoona muziki huu, ndiyo tumeanza ligi sasa. Tunarudia palepale kauli mbiu yetu ‘Nyankumbu hatoki mtu’.”

“Kocha (Hemed Morocco) alituachia programu ya kufanyia kazi, hivyo mtiririko aliotuachia tuliwasimamia vijana, tulijua mapungufu yao, kwa kweli tulikwenda vizuri na program na leo matunda yake yameonekana,” aliongeza Choki, huku nahodha wa timu hiyo, Samwel Onditi alisema ushindi wa mechi iliyopita uliwajengea hali ya kujiamini na njaa ya kutaka kuendelea kushinda, huku akiamini benchi la ufundi liko makini.

Kwa upande wa Namungo wamesema wataendelea pale walipoishia baada ya kutoka kuifyatua Ihefu mabao 2-0 na kuanza kujipata kwenye Ligi baada ya awali kuanza kwa kusuasua ikabla ya kuzinduka hivi karibuni.