Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fredy atabiriwa 'Top Scorer', Kibu asamehewa

Fred Pict
Fred Pict

Muktasari:

  • Awali, Kibu alipewa likizo ya muda na uongozi akaenda Marekani kwa mapumziko kabla ya kurejea nchini na kisha kutimkia Norway kwenda kuzungumza na timu moja ya huko ili imsajili bila idhini ya waajiri wake.

MSHAMBULIAJI wa Simba, Fredy Michael ametabiriwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu ujao, huku Kibu Denis akisamehewa na wana Msimbazi baada ya sakata lake la kutojiunga na kambi ya kikosi hicho iliyofanyika Misri.

Awali, Kibu alipewa likizo ya muda na uongozi akaenda Marekani kwa mapumziko kabla ya kurejea nchini na kisha kutimkia Norway kwenda kuzungumza na timu moja ya huko ili imsajili bila idhini ya waajiri wake.

Akizungumza leo katika kilele cha tamasha la 'Simba Day', Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally kwenye utambulisho wa wachezaji watakaokitumikia kikosi hicho msimu ujao, amesema hakuna upinzani kwamba Fredy atachukua kiatu cha ufungaji bora.

"Haina ubishi bila shida yoyote huyu ndio mfungaji bora msimu huu, atafunga sana Msimbazi," Amesema Ahmed.

Wakati anatabiri hayo kwenye utambulisho, amesema Kibu   wana Simba wamemsamehe kwa kile walichokiita utovu wa nidhamu baada ya kutojiunga na kambi.

 "Sisi kama mashabiki tumekusamehe... ndugu wakigombana shika jembe ukalime, tumemaliza ugomvi na msimu huu bado yupo sana," amesema Ahmed.