Fountain yabanwa na Ceasiaa


MCHEZO wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kati ya Fountain Gate Princess na Ceasiaa Queens ya mkoani Iringa umemalizika katika uwanja wa Jamhuri  kwa timu hizo kutoka sare ya kutofungana.

Licha ya Fountain kuishambulia kwa dakika 90 Ceasiaa lakini Hadi filimbi ya mwisho ya mwamuzi Halima Ally kutoka mkoani Manyara hakuna timu iliyoweza kupata bao.


Zifuatazo ni dondoo muhimu za mchezo huu.

Huu ni mchezo wa tatu kwa Kocha wa Ceasiaa Queens,Mustapha Kayinda  raia wa Uganda,kuiongoza timu hiyo akichukua nafasi ya Emmanuel Masawe.Katika michezo hiyo ameshinda dhidi ya The Tiger  (1-0), amepoteza dhidi ya Yanga Princess 1-0 na sare (0-0)

Huu ni mchezo wa pili kwa kipa wa Fountain Gate, Winfrida Seda raia wa Kenya kuanza langoni ,katika michezo saba iliyocheza timu hiyo,michezo mingine mitano  ameanza  Monica Chebet ambaye ana Cleensheet.

Katika michezo hiyo saba,Fountain  imeruhusu mabao 2 yote katika mchezo dhidi ya Simba Queens uliomalizika kwa Simba  Queens kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Takwimu zinazonyesha Fountain katika mechi nne ilizocheza nyumbani imeshinda mitatu  dhidi ya  Mkwawa Queens ( 2-0) Baobab Queens (1-0) Alliance (4-0)  huku ikitoka  sare ya (0-0) dhidi ya Ceasiaa Queens.

Katika michezo mitatu iliyocheza ugenini imeshinda miwili na kupoteza mmoja.Imeshinda dhidi ya Yanga Princess 1-0 na Amani Queens 4-0 huku ikipoteza dhidi ya Simba Queens kwa mabao 2-1.

Takwimu zinaonesha  Ceasiaa Queens katika michezo saba iliyocheza nyumbani imecheza minne,imeshinda miwili  dhidi ya Tiger (1-0) na Amani Queens (2-1) huku ikipoteza dhidi ya JKT Queens (2-1) na Yanga Princess,(1-0.

Katika michezo  mitatu  miwili  imepoteza dhidi ya Baobab (2-1) na Alliance Girls 1-0 huku ikitoa sare ya kutofungana dhidi ya Fountain.

Timu hizo zinakutana kwa mara ya kwanza katika WPL  baada ya Ceasiaa Queens kubadilisha jina kutoka Ruvuma Queens.

Katika mabao 13 ya Fountain Gate,matano yamefungwa na Mkenya Cynthia Musungu huku matatu yakifungwa Winfrida Gerrald.

Ceasiaa Queens imefunga mabao matano  na kufungwa saba katika michezo saba iliyocheza mpaka sasa.