Fountain Gate Princess bingwa Gate Tournament 2023

Timu ya Fountain Gate Princess imeshinda taji la Gates Tournament baada ya kuifunga Yanga Princess kwa mikwaju ya penalti 9-8 baada ya kumaliza dakika 90 wakifungana bao 1-1.

Mashindano hayo yalikuwa na timu sita za Fountain Gate, Bunda Queens, Gets Program, Yanga Princess, Baobab Queens iliyoshika nafasi ya tatu na New Generation kutoka Zanzibar.

Timu hizo ziliwekwa kwenye makundi A na B ambapo walichuana kwa kucheza mechi mbilimbili kila kundi na leo yamefikia tamati jijini Dodoma yalipofanyika.