Fletcher aiangukia Man United

Friday October 02 2020
man utd pic

London, England. Darren Fletcher ameiangukia Manchester United kumuunga mkono kocha mwenye wakati mgumu, Ole Gunnar Solskjaer kwa kusajili nyota watano wapya.

Kiungo huyo wa zamani wa Mashetani Wekundu mwenye miaka 36, ameishuhudia timu yake ya zamani ikisajili mchezaji mmoja msimu huu hadi sasa.

Donny van de Beek ndiye mchezaji aliyesajiliwa na miamba hiyo ya Old Trafford msimu huu kwa Pauni 39 milioni.

Wakati dirisha la usajili likifungwa Jumatatu, Fletcher anajua kuwa muda hautoshi kwa klabu hiyo kupata kikosi bora cha ushindani msimu huu.

Kiungo huyo aliiambia Sky Sports: “Tunatakiwa kujua kuwa ni ngumu mno kwa Manchester United kusajili. Kuna gharama, makubaliano na ugumu mwingine.

“Lakini wakati huo huo inachanganya sana, kwa Ole, mashabiki, kila mmoja katika klabu, kutokana na ukweli kwamba Chelsea na timu nyingine zimejiimarisha mapema, wanatumia fedha kwa sasa wakati Manchester United ikioneka kusubiri dakika za mwisho.

Advertisement

“Binafsi, Ole Gunnar Solskjaer, kwa kazi anayofanya katika klabu, kutoka alipoanza hadi sasa,anastahili kusajili nyiota anaowataka.

“Siku zote amekuwa akitanguliza maslahi ya klabu, najua, lakini wakati mwingine Ole kujitazama, kwasababu atakuwa akijadiliwa kila msimu.

“Watu hawatatazama kazi uliyofanya, wanataka kuona sasa, kwa Manchester United kufika inapotaka, inahitaji wachezaji wengine wapya.”

Advertisement