Fifa yaikamua Yanga mamilioni

Fifa yaikamua Yanga mamilioni

Muktasari:

WAKATI Simba ikisikilizia kesi yao ya kutakiwa kulipa Sh 294 milioni kwa kosa la kukiuka usajili wa winga wao wa zamani, Shiza Kichuya, Shirikisho la Soka duniani (Fifa) limeshusha rungu jingine kwa watani wao, Simba kwa kutakiwa kulipa zaidi ya Sh 46 milioni.

WAKATI Simba ikisikilizia kesi yao ya kutakiwa kulipa Sh 294 milioni kwa kosa la kukiuka usajili wa winga wao wa zamani, Shiza Kichuya, Shirikisho la Soka duniani (Fifa) limeshusha rungu jingine kwa watani wao, Simba kwa kutakiwa kulipa zaidi ya Sh 46 milioni.

Simba ililimwa fedha hizo baada ya klabu ya Pharco FC ya Misri kulalamika kwa kitendo cha klabu hiyo ya Msimbazi kumsajili na kumtumia Kichuya akiwa na mkataba uliotoka na dili walililofanya mapema mwaka jana ndipo wakapewa siku 45 za kulipa fedha hizo.

Hata hivyo Simba iliomba kupitia hukumu hiyo iliyotokana na maamuzi ya Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya kimichezo na kufanya kusitishwa kwa adhabu hiyo, lakini wenzao Yanga imenyooshwa kupitia nyota wao wa zamani, Amissi Tambwe.

FIFA kupitia mahakama ya michezo CAS imeiamuru Yanga kumlipa Tambwe, Dola 20,000 ambazo ni zaidi ya Sh 46 milioni za Kitanzania.

Yanga imetakiwa kumlipa Tambwe pesa hizo ambazo ni deni la ada ya usajili na mishahara ya miezi mitatu ndani ya siku 45 tangu hukumu hiyo itolewe Desemba 1, 2020.

Imeelezwa baada ya hukumu hiyo, Yanga iliandikiwa barua Desemba 4 ya kuwataka walipe pesa hiyo ndani ya siku 45 vinginevyo watazuiwa kusajili msimu ujao.

Mwanasheria wa Tambwe aliyesimamia kesi hiyo, Felix Majani alikiri imeshinda kesi yao na sasa wanasubiri kulipwa pesa za mteja kutoka Yanga.

“Ndio tumeshinda kesi na tayari tumewaandikia Yanga barua ya kuwataka walipe kile wanachodaiwa, wasipolipa tutarudi FIFA. Imepewa siku 45 za kutulipa na wasipofanya hivyo basi watazuiwa kusajili, kwahiyo tunasubiri kuona nini ambacho kitatokea,” alisema Majani.

Hata hivyo hakuna kiongozi wa Yanga aliyethibitisha taarifa hiyo, licha ya kutafutwa kwa njia ya simu zao za mkononi, kwani simu zao zilikuwa zikiita bila kupokelewa ikiwamo ya Ofisa Habari wao, Hassan Bumbuli.