Fei Toto: Tunawaahidi ushindi, Watanzania watuombee dua

Kiungo wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' baada ya kutua nchini Misri amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu maandalizi ya mechi dhidi ya Uganda kufuzu Afcon 2023.

Fei Toto akihojiwa na kituo cha televisheni cha Azam amesema wamejiandaa vizuri na wanaahidi ushindi kwa watanzania.

"Kweli kuna wachezaji wapya na mwalimu mpya ila Uganda tunawaheshimu ni timu nzuri ina wachezaji wazuri, ila tutaipambania Taifa Stars ili tupatematokeo,"

Ameongeza; " Katika mechi mbili watuombee dua na tutapata matokeo kwa uwezo wake Mungu,"

Taifa Stars itacheza mechi mbili na Uganda ikianzia ugenini Misri Machi 24 na kurudiana Machi 28 jijini Dar.