Fei Toto aomba kuchangiwa fedha aende CAS

Muktasari:

  • Katika barua ambazo zimevuja iliyoelekezwa kwa Feisal, Mei 16 alipokea barua ya malalamiko kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo ikimtuhumu kwa makosa mbalimbali ya kinidhamu.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Feisal Salum kwa mara ya kwanza leo ameomba watanzania na wapenzi wa soka kumchangia fedha ili aende Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa ya michezo CAS

Fei Toto ametuma maombi hayo kwenye mtandao wake wa Instagram anasema "Ndugu zangu Watanzania na familia yote ya soka kwa Bara na visiwani. Mimi kijana wenu ambaye kwa miaka yote nimekua na nidhamu nje na ndani ya uwanja na kwa dhati nimeitumikia klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania na Zanzibar Heros".

"Utiifu wangu umekua shubiri ya maisha yangu ya soka, nimevumilia nimeshindwa, sitamani tena mama yangu kutukanwa. TFF imeshindwa kunisaidia kupata haki yangu ya Kuvunja mkataba na Yanga hivyo nimeamua Kwenda Mahakama ya michezo CAS".

"Nahitaji Mchango wa kila Mtanzania mpenda haki na maendeleo ya wachezaji wa Kitanzania ambao wamekua kimya na woga juu ya maslahi, Heshima na Haki zao. Naomba unichangie kadiri utakavyoweza ili niweze kupata pesa ya Kulipia gharama za kufungua Jalada la kesi yangu CAS ili kupata Haki yangu ya Kuondoka Yanga kwa kuvunja mkataba".

"Tafadhali naomba unichangie ili nipate haki yangu itakayoniwezesha kutumikia kipaji changu na Timu za Taifa (Tanzania na Zanzibar) katika namna tofauti kwa manufaa yangu na Taifa. Shangazi Fatma Karume na wanasheria wengine watafanya kazi Bure".

Katika barua ambazo zimevuja iliyoelekezwa kwa Feisal, Mei 16 alipokea barua ya malalamiko kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo ikimtuhumu kwa makosa mbalimbali ya kinidhamu.