Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Federer agoma kupokea Dola 1 milioni za Saudi Arabia

Muktasari:

  • Federer alisema wazi kuwa ameikataa ofa hiyo kutokana na utawala wa Saudi Arabia kukiri kumuua kinyama mwandishi wa habari raia wa nchi hiyo Jamal Khashoggi, aliyekuwa akiishi nchini Uturuki.

Paris, Ufaransa. Mcheza tenisi mahiri wa Uswisi, Roger Federer, ameipuuza na kukataa ofa ya Dola 1 milioni kutoka Serikali ya Saudi Arabia ili kucheza mechi za mashindano maalumu ‘Super Match’.

Wakati Federer anayeshika namba tatu kwa ubora duniani akiipiga chini ofa hiyo, fedha hizo zimewatoa udenda nyota namba moja Rafael Nadal raia wa Hispania na namba tatu Novak Djokovic raia wa Serbia, ambao wamkubali mwaliko huo.

Khashoggi aliuawa na kundi la majasusi kutoka Saudi Arabia alipoenda kwenye ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul, kuchukua nyaraka kwa ajili ya kufunga ndoa na mchumba wake wiki chache zilizopita.

Mwandishi huyo ameuawa kutokana na kinachoaminika kuukosoa mara kwa mara utawala wa kimabavu unaofanywa na Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud ambnaye anaiongoza nchi hiyo tangu Januari 23, 2015.

Hata hivyo kutokana na kushutumiwa na jamii ya kimataifa Nadal na Djokovic wamedai kuwa walisaini mkataba wa kushiriki mchezo huo maalumu mwaka mmoja uliopita.

Wachezaji hao wapo jijini Paris wakijiandaa kwa Paris Masters na wamedai kuwa wataangalia hali ya mambo ilivyo kabla ya kufanya uamuzi kama washiriki ama wasishiriki mashindano hayo maalumu.