Eritrea yaitupa nje Kenya kwa mshangao

Muktasari:
Kenya ilitwaa ubingwa wa mashindano ya Chalenji mwaka 2017 baada ya kuifunga Zanzibar kwa mikwaju ya penati 3-2 baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 katika dakika za kawaida za mchezo.
KENYA imevuliwa kwa aibu ubingwa wa mashindano ya Chalenji baada ya kupewa kichapo cha mabao 4-1.
Pamoja na kuingia katika mechi hiyo huku ikipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi baada ya kutamba kundi B, Kenya ilijikuta ikizidiwa vilivyo katika mechi hiyo na kujikuta ikishambuliwa tangu dakika za mwanzoni za mechi.
Mkosi kwa Kenya ulianzia dakika ya 19 baada ya mshambuliaji wake Oscar Wamalwa kujifunga wakati alipokuwa akijaribu kuokoa shambulizi la Eritrea.
Bao hilo lilidumu hadi muda wa mapumziko na dakika nne tu baada ya kipindi cha pili kuanza, Abel Okbay aliipatia timu yake bao la pili lakini ikawachukua Kenya dakika nne tu kupata bao la kwanza kupitia Oscar Wamalwa.
Jitihada za Kenya kusawazisha mabao hayo zilizimwa dakika ya 68 na 74 baada ya Eritrea kufunga mabao mengine mawili kupitia Okbay na Robel Teklemichael