Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Elifadhili: Ndoto yangu haijatimia

Alfadhili Pict

Muktasari:

  • Elifadhili mmoja wa waandamizi wa kikosi hicho, ametolewa kikosini akiwa na mkongwe mwenzake Salum Kimenya wakisubiri kupangiwa majukumu mengine.

ALIYEKUWA beki wa kati na nahodha wa Tanzania Prisons, Jumanne Elifadhili amesema licha ya kuondolewa kikosini, lakini hesabu zake zilikuwa ni kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu, huku akieleza kuwa huenda akaibukia timu nyingine kwani ndoto yake haijatimia.

Elifadhili mmoja wa waandamizi wa kikosi hicho, ametolewa kikosini akiwa na mkongwe mwenzake Salum Kimenya wakisubiri kupangiwa majukumu mengine.

Beki huyo aliyejiunga na Maafande hao tangu 2012/13, alikuwa tegemeo na atakumbukwa kwa upambanaji akiwa sehemu ya walioipandisha timu hiyo msimu huo na kuinusuru kushuka daraja 2022/23 walipocheza ‘playoff’ dhidi ya JKT Tanzania na kushinda jumla ya mabao 2-1.

Akizungumza na Mwanaspoti, Elifadhili alisema malengo yalikuwa ni kustaafu mwishoni mwa msimu huu, hivyo ndoto yake haijatimia akieleza kuwa huenda akaibukia timu nyingine msimu ujao.

Alisema kwa muda aliowatumikia Wajelajela hao, yapo machungu na tamu aliyopitia lakini zaidi ni kufika kikosini timu inashuka daraja, lakini presha waliyokutana nayo wakati wa kuinusuru kushuka daraja.

“Nilikuwa nistaafu mwisho wa msimu huu, hivyo ndoto haijatimia, japokuwa ni muajiriwa wa Jeshi la Magereza lakini naweza kuibukia timu nyingine hata msimu ujao kwa kuwa lolote linawezekana,” alisema nyota huyo.

Kuhusu mwenendo wa timu alivyoiacha, staa huyo asiye na maneno mengi amesema hawezi kuongea zaidi badala yake anaiombea matokeo mazuri kuhakikisha inabaki Ligi Kuu kwa kumaliza nafasi nzuri.

Prisons haikuwa na mwanzo mzuri ikiwa chini ya Kocha Mbwana Makata ambaye alisitishiwa mkakataba na sasa amekabidhiwa mikoba, Aman Josiah aliyetokea Geita Gold inayoshiriki Ligi ya Championship. Kwa sasa Prisons inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 14 baada ya kucheza mechi 16.

Timu hiyo yenye makazi yake mitaa ya Ruanda jijini Mbeya, ilikuwa ikitamba na mastaa wake wakongwe akiwamo Elifadhili, Kimenya, Samson Mbangula, Jeremiah Juma, Michael Ismail, Nurdin Chona na Benjamin Asukile aliyestaafu msimu uliopita na wote ni waajiriwa wa Jeshi la Magereza.