Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Bigman, Katwila waitana mezani

BIGMAN Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Gao alisema licha ya kutotimiza malengo ya kupanda Ligi Kuu Bara msimu ujao, ila wameridhishwa na mwenendo wa timu hiyo, hivyo wanataka kuweka mikakati mapema kusuka kikosi hicho.

RAIS wa Bigman FC, Ahmed Waziri Gao, amesema baada ya msimu kuisha watakaa chini na kocha wa timu hiyo, Zubery Katwila kwa lengo la kujua hatima yake katika kikosi hicho kwa msimu ujao, baada ya mkataba wake aliousaini kufikia rasmi ukomo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Gao alisema licha ya kutotimiza malengo ya kupanda Ligi Kuu Bara msimu ujao, ila wameridhishwa na mwenendo wa timu hiyo, hivyo wanataka kuweka mikakati mapema kusuka kikosi hicho.

“Malengo yetu ya kwanza yalikuwa ni kuhakikisha timu inabaki Championship na hilo tumefanikiwa, kwa sasa tunajipanga kwa msimu ujao, ambao tunataka kuboresha kikosi zaidi kwa kuanzia na benchi letu la ufundi lililopo,” alisema Gao.

Kocha huyo mzoefu aliyetamba na timu mbalimbali zikiwemo, Ihefu ambayo kwa sasa ni Singida Black Stars na Mtibwa Sugar, alijiunga na Bigman akichukua nafasi ya Fredy Felix ‘Minziro’, aliyejiunga na Pamba kuchukua mikoba ya Goran Kopunovic.

Timu hiyo zamani iliyofahamika kama Mwadui FC ikihamia Lindi, katika mechi 29 ilizocheza kabla ya ile ya jana dhidi ya TMA FC, imeshinda 12, sare 11 na kupoteza sita, ikifunga mabao 28 na kuruhusu 19, ikishika nafasi ya nane na pointi 47.