Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dube ashindwa kujizuia, achekelea taji Ligi Kuu Bara

DUBE Pict

Muktasari:

  • Lakini msimu huu wa 2024/25, hatimaye Prince Dube, mshambuliaji kutoka Zimbabwe, amevuna alichokipanda akiwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichotwaa ubingwa wa ligi kwa kishindo.

KWA miaka minne alicheza katika Ligi Kuu Bara akiwa na Azam FC. Msimu baada ya msimu, ndoto yake ya kutwaa ubingwa iliendelea kuwa mbali licha ya juhudi kubwa alizoweka uwanjani. 

Lakini msimu huu wa 2024/25, hatimaye Prince Dube, mshambuliaji kutoka Zimbabwe, amevuna alichokipanda akiwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichotwaa ubingwa wa ligi kwa kishindo.

Dube, aliyesajiliwa na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea Azam, amethibitisha kuwa maamuzi sahihi hutoa matunda bora. 

Katika msimu wake wa kwanza tu akiwa na Wananchi, amefunga mabao 13 akicheza kwa kiwango bora na kuwa sehemu ya mafanikio makubwa ya klabu hiyo iliyotwaa ubingwa ligi kwa pointi 82.

“Nina furaha sana baada ya ndoto yangu kutimia hapa Tanzania. Medali ya ubingwa wa Ligi Kuu ilikuwa ndoto yangu tangu naingia hapa nchini, na sasa imetimia.”

Aliongeza, ushindi huu si wa kwake peke yake bali pia ni historia ya kipekee kwa familia yake na nchi yake ya Zimbabwe.

“Hii itacha historia kubwa kati yangu mimi, Tanzania na klabu hii ya Yanga! Mimi nimefurahi na kama unavyoona pia familia yangu imefurahi sana.”

Dube alijiunga na Azam mwaka 2020 akitokea Highlanders FC ya Zimbabwe na kuonyesha ubora wake kwa kufunga mabao muhimu kila msimu, lakini hakuwahi kuonja ubingwa wa Ligi Kuu Bara. 

Ndoto hiyo ilikuwa ngumu wakati huo, hasa kwa kuwa Azam ilikosa uthabiti wa kiushindani dhidi ya miamba ya jadi Yanga na Simba.

Sasa akiwa sehemu ya Yanga, Dube si tu ametwaa ubingwa, bali pia ameimarika zaidi kama mchezaji, akishirikiana vyema na washambuliaji wenzake kama Clement Mzize na Pacome Zouzoua na kutengeneza miongoni mwa safu kali zaidi za ushambuliaji.

Tangu aanze kucheza Ligi Kuu Bara, Dube amefunga jumla ya mabao 47, yakiwamo 13 ya msimu huu akiwa na Yanga na mengine 34 wakati akiitumikia Azam aliyoichezea misimu minne na msimu wa kwanza alifunga mabao 14, wa pili alifunga moja kutokana na kuwa majeruhi wa muda mrefu.

Msimu wa tatu alifunga mabao 12 na msimu uliopita aliyoutumikia nusu kabla ya kuanzisha mgomo baridi na kung'oka Chamazi alifunga mabao saba, mbali na mabao ya michuano mingine ya Kombe la Shirikisho(FA) na ile ya kimataifa na asisti zilizozalisha mabao kwa timu zote mbili hadi leo hii.