Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dodoma Jiji ‘top four’ yayeyuka, sasa yawinda heshima

Muktasari:

  • Dodoma Jiji ilianza na mzuka msimu huu ikitabiriwa kuwa kwenye timu zinazoweza kumaliza nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, lakini kwa sasa ndoto hiyo imeyeyuka rasmi.

BAADA ya hesabu za ‘Top Four’ Ligi Kuu Bara kukwama, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Aman Josiah amekubali yaishe, huku akizipigia hesabu mechi nne zilizobaki kusaka heshima, huku akiwapa tano nyota wa kikosi hicho.

Dodoma Jiji ilianza na mzuka msimu huu ikitabiriwa kuwa kwenye timu zinazoweza kumaliza nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, lakini kwa sasa ndoto hiyo imeyeyuka rasmi.

Hii ni baada ya Singida Black Stars kufikisha pointi 44 na mtaji wa mabao manane katika nafasi ya nne, huku Dodoma Jiji ikiwa na pointi 33 ikidaiwa mabao manne ikikamata nafasi ya nane, timu zote zikiwa na michezo minne kumaliza msimu.

Kwa sasa Dodoma Jiji imebakiza mechi dhidi ya Singida Black Stars itakayopigwa Juni 17 ugenini, kisha kuwakaribisha JKT Tanzania na Mbeya City, itamaliza ligi ugenini mbele ya Azam.

Akizungumza na Mwanaspoti, Josiah ambaye ni msimu wake wa pili Ligi Kuu akiwa Kocha Mkuu, alisema matokeo ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons, ulififisha ndoto zao za kuitaka nafasi ya nne.

Alisema kwa sasa hesabu zilizobaki ni kupambania ushindi kwenye mechi nne ili kusaka heshima ya kumaliza nafasi nzuri na anachojivunia ni ubora wa kikosi chake kwenye upambanaji.

“Kimahesabu ndoto za nafasi ya nne ni ngumu lakini lolote linawezekana, kimsingi tunaenda kujipanga na michezo iliyobaki kupambania heshima ya ushindi na kuwa nafasi nzuri,” alisema Josiah.

Kuhusu ubora wa nyota wake, kocha huyo aliyewahi kuzinoa Biashara United ya Mara, Tunduru Korosho ya Ruvuma na Tanzania Prisons ya Mbeya, hakusita kuwapongeza mastaa wake kwa kiwango bora wanachoonesha uwanjani.

Alisema kwa sasa nyota wake wana uwezo mkubwa na wamekuwa sehemu kubwa ya mafanikio kwa timu hiyo kutokana na kiwango cha mmoja mmoja wanachoonesha uwanjani.

“Kwa ujumla niwapongeze wachezaji wangu wamekuwa sehemu ya mafanikio kutokana na kiwango wanachoonesha na wamekuwa makini kufuata maelekezo na ndio siri kubwa ya kutuona katika hali hii,” alisema kocha huyo.