Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Corona yawakutanisha Deo Kanda wa Simba SC na Shikhalo wa Yanga

Muktasari:

Wakati wakisalimiana Kanda alianza kumwelezea Shikhalo anayetokea Kenya kwamba katika mchezo baina yao uliopigwa Januari 4 na kumalizika kwa sare ya 2-2 kama isingekuwa kipa huyo basi timu yake ingeondoka na mabao mengi ya aibu.

Dar es Salaam. NANI aliyekuambia Simba na Yanga ni mahasimu? Klabu hizi ni watani na wapinzani wa jadi wa soka nchini, ndio maana hata mashabiki wao wanajichanganya pamoja wanapotoka viwanjani na mambo yakawa poa tu mitaani tofauti na baadhi ya wapinzani wa jadi wa nchi nyingine.
Sasa kumbe utamaduni huo, upo hata kwa wachezaji kwani unaambiwa kipindi hiki, timu zikiwa mapumzikoni kupisha ugonjwa wa Corona, mastaa wiwili wa kigeni wa Simba na Yanga, Deo Kanda na kipa Farouk Shikhalo walijkutana chemba na kupiga stori mbili tatu za kusisimua.
Wawili hao walikutana hivi karibuni katika moja ya gym wakifanya mazoezi ya kujiweka sawa ambapo ghafla kila mmoja akamkumbuka mwenzake jinsi walivyokutana mara ya mwisho katika mchezo baina ya timu hizo.
Wakati wakisalimiana Kanda alianza kumwelezea Shikhalo anayetokea Kenya kwamba katika mchezo baina yao uliopigwa Januari 4 na kumalizika kwa sare ya 2-2 kama isingekuwa kipa huyo basi timu yake ingeondoka na mabao mengi ya aibu.
Mkongomani huyo aliongeza, Shikhalo ni kipa anayejua kulipunguza lango akiwa mzuri pia katika hesabu ya kuokoa mashuti huku akishangaa kwanini sasa hamuoni akidaka tena.
“Ulifanya kazi sana ile mechi kwangu mimi ulistahili kuwa mchezaji bora wa mchezo kama usingekwa wewe siku ile tungewafunga nyingi sana uliwaokoa sana Yanga, nashangaa sasa huchezi unaumwa?” Kanda alimhoji Shikhalo, huku mwandishi akiwa shuhuda wa stori zao hizo.
Naye Shikhalo ambaye muda wote alikuwa akicheka na kusema asante alimjibu mshambuliaji huyo mkongwe, hata yeye anamkubali Kanda na kwamba bao la pili alilomfunga katika mchezo huo alijiua kutulia na kuchagua goli vyema.
Shikhalo alisema kama angekuwa mshambuliaji mwenye papara angepata wakati mgumu kufunga kwa jinsi alivyokuwa amejipanga lakini akashangaa kuona Kanda amechagua sehemu bora na kufunga kirahisi.
“Nashukuru kaka lakini hata wewe ni mshambuliaji mzuri sana pale ulidhihirisha kwamba una uzoefu wa kutosha vile ulivyofanya,” alijibu Shikhalo.