Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Coastal Union yaanza na Chikola, Bwenzi

COASTAL Pict

Muktasari:

  • Coastal Union imeanza na wachezaji hao ikiamini kwamba ikikamilisha kuwasajili watasaidia timu kufanya vizuri msimu ujao kufuatia sasa kushika nafasi ya 10 ikiwa inapambana kutoka kwenye mtego wa kutocheza play off ya kuepuka kushuka daraja.

WAKATI msimu huu ukielekea ukingoni, klabu mbalimbali zinazoshiriki Ligi Kuu Bara zimeanza hesabu mapema za kuimarisha vikosi vyao kwa ajili ya msimu ujao ambapo inaelezwa Coastal Union imefanya mazungumzo na nyota wawili, Offen Chikola wa Tabora United na Seleman Bwezi anayecheza KenGold.

Coastal Union imeanza na wachezaji hao ikiamini kwamba ikikamilisha kuwasajili watasaidia timu kufanya vizuri msimu ujao kufuatia sasa kushika nafasi ya 10 ikiwa inapambana kutoka kwenye mtego wa kutocheza play off ya kuepuka kushuka daraja.

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Coastal Union, zinabainisha kwamba timu hiyo ina mipango ya kuimarisha maeneo mengi ya kikosi kwa msimu ujao, lakini kwa kuanzia ni eneo la mbele baada ya kugundua haikufanikiwa kufunga mabao mengi msimu huu kwani imetikisa nyavu za wapinzani mara 24 katika mechi 28.

“Coastal Union imeanza kufanya mazungumzo na mastaa hao wawili, ila kwa upande wa Offen Chikola, imefikia kwenye hatua nzuri huku suala la Bwenzi mambo yakiwa bado magumu.

“Bwenzi ametaka dau kubwa ambalo Coastal Union haijakubaliana nalo, hiyo imetokana na kiwango alichoonyesha licha ya KenGold kushuka daraja na kufanya kutakiwa na timu nyingi,” kilisema chanzo hicho.

Hivi karibuni, Mwanaspoti liliripoti kwamba Yanga imeanza kufanya mazungumzo na Chikola ambaye amekuwa na kiwango bora msimu huu ndani ya Tabora United akifunga mabao saba na asisti mbili ndani ya ligi na tayari imempa mkataba wa awali.

Kwa upande wa Bwenzi ambaye alitua KenGold dirisha dogo msimu huu akitokea Mbeya Kwanza, ameweka rekodi ya kufunga mabao matano na asisti moja kwenye ligi. Wachezaji hao wote wanamaliza mikataba yao msimu huu kwenye timu wanazozitumikia.

Kwa sasa timu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu zimebakiza mechi mbili kumaliza msimu, huku michezo ya mwisho ikitarajiwa kuchezwa Juni 22.

Coastal Union ambayo msimu uliomalizika ilikuwa nafasi ya nne na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, sasa iko namba 10 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 31, ikishinda mechi saba, sare 10 na kupoteza 11.