Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chukwu: Ubora umenirudisha Singida

Chuku Pict

Muktasari:

  • Chukwu ambye alitua Bongo msimu uliopita na kuanza kuichezea Singida huku akiwa na mkataba wa miaka miwili, alitolewa kwa mkopo kwenda Ihefu (sasa Singida Black Stars) kisha msimu huu akapelekwa tena Tabora United kwa mkopo kabla ya dirisha dogo kurudi Singida.

KIUNGO wa zamani wa Rivers United ya Nigeria, Morice Chukwu anayeichezea Singida Black Stars, amesema kuwa kurejea katika kikosi hicho kunadhihirisha ubora alionao.

Chukwu ambye alitua Bongo msimu uliopita na kuanza kuichezea Singida huku akiwa na mkataba wa miaka miwili, alitolewa kwa mkopo kwenda Ihefu (sasa Singida Black Stars) kisha msimu huu akapelekwa tena Tabora United kwa mkopo kabla ya dirisha dogo kurudi Singida.

Akizungumza na Mwanaspoti, Chukwu alisema amerejea ndani ya kikosi hicho kutokana na maelewano mazuri aliyokuwa nayo na mabosi zake lakini pia ubora aliouonyesha akiwa Tabora United.

Alisema kuwa, urahisi aliokuwa nao ndani ya kikosi hicho ni kwamba wachezaji wengi waliopo alishawahi kucheza nao kabla hajaondoka.

“Nimerudi tena kwa sababu awali mimi na mabosi zangu tulikuwa na kutokuelewana kidogo ila kwa sasa kila kitu kipo sawa.

“Sio jambo geni kurudi Singida kwani nilishacheza Ihefu, katika kucheza kwangu kote kuna kitu kimeongezeka ikiwemo kiwango ndio maana nimerudi,” alisema na kuongeza:

“Kitu pekee ni kwamba hakuna utofauti wa wachezaji waliopo na niliowaacha kwani ni wale wale kama Marouf Tchakei na Elvis Rupia. Najua nitakutana na changamoto ila ninaamini kuwa mimi ni mchezaji bora.”