Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chukwu mipango imetimia Singida BS

Muktasari:

  • Huu ni msimu wa pili Chukwu anacheza soka nchini Tanzania akitokea Rivers United ya Nigeria ambayo msimu wa 2022/23 ilicheza dhidi ya Yanga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika yeye akiwemo.

KIUNGO wa Singida Black Stars, Morice Chukwu raia wa Nigeria, amesema mipango ya klabu hiyo msimu huu inaendelea kutimia, huku akipiga hesabu za kimataifa mapema.

Huu ni msimu wa pili Chukwu anacheza soka nchini Tanzania akitokea Rivers United ya Nigeria ambayo msimu wa 2022/23 ilicheza dhidi ya Yanga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika yeye akiwemo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Chukwu alisema kwa sasa mipango ya timu hiyo iko mbioni kufikia malengo waliyojiwekea kwani wanachokipambania sasa ni kuishusha Azam FC nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

“Ujue Singida ina wachezaji wengi wenye uzoefu na michuano ya kimataifa, lakini sio hivyo tu hata ubora wa timu kwa ujumla unaonyesha jinsi tunavyostahili kushiriki mashindano hayo.

“Sio jambo jipya kwetu kushiriki michuano ya CAF, misimu miwili nyuma tulijaribu ila hatukufanikiwa, ila sasa naamini tutafika mbali zaidi.

“Tunahitaji morali pekee kutoka kwa mashabiki na mabosi wetu wa klabu ili tuweze kujiamini zaidi, bila kusahau mazoezi bora kufikia malengo, tunataka kumaliza ligi nafasi ya tatu,” alisema Chukwu.

Singida Black Stars yenye uhakika wa kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao kutokana na nafasi inayoshika kwenye msimamo wa ligi, inachuana na Azam FC iliyopo nafasi ya tatu na pointi 57 baada ya kucheza mechi 28, huku yenyewe ikicheza michezo 27 ikiwa na pointi 53.