Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chobanka afichua kilichoiangusha Ceasiaa

CHOBANKA Pict

Muktasari:

  • Chobanka amesema timu imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kukuza vipaji vya wachezaji, lakini baada ya kung’€ara wengi wao huondoka na kujiunga na klabu nyingine zenye uwezo mkubwa kifedha, jambo linalowalazimu kuanza upya kila msimu.

KOCHA Mkuu wa Ceasiaa Queens, Ezekiel Chobanka amesema kubadilisha kikosi kila msimu ndicho kilichochangia timu hiyo kushindwa kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania msimu huu tofauti na ilivyokuwa katika misimu miwili iliyopita.

Chobanka amesema timu imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kukuza vipaji vya wachezaji, lakini baada ya kung’€ara wengi wao huondoka na kujiunga na klabu nyingine zenye uwezo mkubwa kifedha, jambo linalowalazimu kuanza upya kila msimu.

Akizungumza na  Mwanaspoti, kocha huyo amesema kukosekana kwa muendelezo wa kikosi kumeathiri ushindani wa timu hiyo.

“Moja ya sababu kubwa iliyotufanya tusifanye vizuri msimu huu ni kubadilisha wachezaji kila mwaka. Tunawakuza, wanakuwa na kiwango kizuri halafu wanaondoka kwenda timu nyingine mwishowe tnaanza tena kujenga kikosi kipya’,’€amesema Chobanka.

Aliongeza kuwa misimu miwili iliyopita timu ilikuwa na mwendelezo mzuri wa kupata matokeo jambo lililowapa ushindani mkubwa, lakini hali imekuwa tofauti msimu huu.

‘‘Kukibadilisha kikosi mara kwa mara ni vigumu kupata matokeo ya haraka. Inahitaji muda kwa wachezaji kuzoeana na kuelewana ndani ya uwanja tunashukuru tunasalia msimu ujao lakini hatukufanya vizuri’,’  ameeleza.

Kocha huyo amesema kama benchi la ufundi tayari wamepanga kukaa na viongozi wa klabu mara baada ya msimu kumalizika ili kujadili namna ya kuwabakiza wachezaji muhimu na kuimarisha maeneo yenye upungufu.

Anaamini endapo klabu itafanikiwa kujenga msingi wa kikosi na kuongeza wachezaji wachache wa kuimarisha timu, Ceasiaa Queens itakuwa na uwezo wa kurejea kwenye ushindani mkubwa msimu ujao.

"Tukifanikiwa kuwabakiza wachezaji wetu muhimu na kufanya maboresho machache, ninaamini tutakuwa na timu nzuri zaidi msimu ujao. Tutakaa na uongozi kuzungumzia hilo kwa sababu ndiyo njia ya kujenga timu yenye ushindani,"  amesema Chobanka.


Msimu wa 2024/25 timu

Kauli hiyo inaonyesha changamoto inayozikabili klabu nyingi za soka la wanawake nchini, ambapo kuhama kwa wachezaji kila mwisho wa msimu kunafanya baadhi ya timu kushindwa kuwa na muendelezo mzuri wa kiwango na kulazimika kuanza upya mchakato wa kujenga kikosi.