Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

 Simba Queens, Yanga Princess zampa akili kocha Ceasiaa

KOCHA Pict

Muktasari:

  • Ceasiaa iko nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi na katika mechi 15, imeshinda tatu, sare tatu na kupoteza tisa ikikusanya pointi 12.

KAIMU Kocha Mkuu wa Ceasiaa Queens, Sultan Juma amesema kukutana na Simba Queens na Yanga Princess ni somo kubwa kwa kikosi chake licha ya kupoteza michezo hiyo.

Sultan ambaye aliachana na Alliance Girls dirisha dogo la usajili, kwa sasa yupo Ceasiaa kama kaimu kocha mkuu akishika nafasi ya Ezekiel Chobanka ambaye yupo masomoni.

Sultan amesema timu hiyo imepata nafasi ya kucheza dhidi ya Simba Queens, JKT Queens na Yanga Princess, huku akisisitiza  uzoefu wa timu hizo umeonekana kwa tofauti kubwa.

“Nizipongeze timu kubwa, kuna wakati uzoefu unaamua matokeo. Kikubwa tumepoteza dhidi yao, lakini tumejifunza mambo mengi sana,” amesema Sultan.

Kocha huyo alibainisha changamoto walizokutana nazo zimekuwa darasa muhimu kwa wachezaji wake, hasa katika kuboresha viwango na ushindani wao kwenye ligi.

“Kwanza nashukuru kwa mapumziko tuliyoyapata, tunaamini yatatusaidia kurekebisha mapungufu yetu na kurudi tukiwa bora zaidi,” amesema.

Kwenye mzunguko wa pili timu hiyo ilipoteza dhidi ya JKT kwa mabao 4-0 na Simba bao 1-0, huku kwa Yanga ikiambulia kichapo cha mabao 4-0 mzunguko wa kwanza.

Ceasiaa iko nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi na katika mechi 15, imeshinda tatu, sare tatu na kupoteza tisa ikikusanya pointi 12.