Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chipukizi kuja kivingine msimu ujao

CHIPUKIZI Pict

Muktasari:

  • Msimu huu wa 2025-2026, Chipukizi imejikuta ikipoteza tena fainali ya michuano hiyo mbele ya KMKM kama ilivyokuwa msimu wa 2024-2025 dhidi ya mpinzani huyohuyo.

BAADA ya kuchezea vipigo kwenye fainali mbili mfululizo za Kombe la FA Zanzibar, Chipukizi imesema itajipanga vizuri msimu ujao ili kuondoa hali hiyo na hatimaye kubeba ubingwa.

Msimu huu wa 2025-2026, Chipukizi imejikuta ikipoteza tena fainali ya michuano hiyo mbele ya KMKM kama ilivyokuwa msimu wa 2024-2025 dhidi ya mpinzani huyohuyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Habari wa Chipukizi, Kheri Kidema amesema hakuna aliye tayari kupoteza mechi hasa fainali, lakini siku hiyo ilikuwa ngumu kwani walishindwa kuwazuia wapinzani wao.

“Malengo yetu yalikuwa kuchukua ubingwa wa FA Zanzibar ili tushiriki michunao ya kimataifa, ndiyo maana tulipambana kufanikisha hilo japokuwa tulishindwa,” amesema.

CHIPU 02

Amesema baada ya msimu uliopita kupoteza fainali mbele ya KMKM, safari hii walihitaji kulipa kisasi kupitia mchezo huo, lakini haikuwezekana.

Fainali ya msimu huu iliyochezwa Juni 27, 2026 kwenye Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba, Chipukizi ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya KMKM.

Kabla ya hapo, fainali ya msimu uliopita 2024-2025, Chipukizi ilifungwa mabao 4-2 dhidi ya KMKM kwenye Uwanja Mao Zedong kisiwani Unguja.

CHIPU 01

Kidema aliwaomba mashabiki wa timu ya Chipukizi United na wapenzi wa soka kisiwani Pemba kuendelee kuipa sapoti timu hiyo kwa kila hatua.