Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

China aipa mchongo Taifa Stars

Muktasari:

  • Nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Athumani China, amesema Tanzania inatakiwa kujipanga kwa fainali za Afrika za mwaka 2021.
  • Kwa sasa Kocha Emmanuel Amunike anatakiwa kuandaa programu ya muda mrefu ili kupata wachezaji bora watakaoshindana katika mechi za kufuzu fainali za Afrika 2021.

Dar es Salaam. Kiungo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Athumani China, amefunguka kuhusiana na uamuzi wa Rais John Magufuli kuwaalika wachezaji wa timu hiyo Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Magufuli aliialika Taifa Stars, Ijumaa iliyopita ambapo alizungumza na wachezaji na aliwataka kucheza kufa au kupona kupata ushindi katika mechi zijazo dhidi ya Lesotho Novemba 16 na Uganda Machi 22, mwakani.
Akizungumza jana, China anayeishi nchini Uingereza, alisema anaamini uamuzi wa Rais Magufuli aliyeichangia Taifa Stars Sh50 milioni, utaongeza morali kwa wachezaji kujituma ili kupata ushindi.
Hata hivyo, China alisema Watanzania wasikate tamaa endapo Taifa Stars itakosa tiketi ya kwenda Cameroon kushiriki fainali hizo mwakani.
Badala yake alitoa rai kwa wadau wa soka kuandaa wachezaji ambao watacheza kwa ufanisi mechi za kufuzu fainali za Afrika mwaka 2011 na Kombe la Dunia 2022 zitakazofanyika Qatar.
China alisema mpira ni sayansi duniani kote na Tanzania inatakiwa kujipanga kikamilifu kwa kuandaa program maalumu kuanzia ngazi ya vijana ili kupata timu imara ya kushinda katika mechi za kufuzu fainali hizo.
Kiungo huyo nyota anasoma Shahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha West London, baada ya kuhitimu masomo ya Biashara, Uongozi na Usimamizi wa Fedha katika Chuo Kikuu cha Northampton, alisema Tanzania haipaswi kutegemea vipaji pekee ili kupata timu imara ya ushindani wa kimataifa.
“Hatuwezi kufanikiwa kwa kutegemea vipaji pekee vya wachezaji, kukua kwa sayansi na teknolojia imesababisha mchezo wa mpira utegemee zaidi maandalizi.
“Sayansi na teknolojia ndiyo hitaji la mchezo wenyewe, mpira kwa sasa ni biashara kubwa duniani, kama ukifanya biashara lazima uhakikishe mara kwa mara unafanya utafiti kupitia wataalamu, ili kuhakikisha unaibua bidhaa mpya zinazozalishwa na kiwanda chako au kuzifanyia maboresho bidhaa zake za zamani kukidhi hitaji la soko,” alisema China.
Alisema vipaji vilivyopo vikiandaliwa nchi itafika mbali kimataifa na hakuna sababu ya kusubiri kupata vipaji kama ilivyokuwa kwa akina Hamisi Gaga (marehemu), Abdallah Kibadeni na Sunday Manara ambao ni baadhi ya nyota waliowika enzi zao.
Naye kiungo wa zamani wa Tukuyu Stars, Yanga na Taifa Stars, ambaye kwa sasa ni kocha, Sekilojo Chambua, alisema kauli ya Rais Magufuli itaongeza hamasa kwa wachezaji na pengine kuiwezesha timu hiyo kufuzu fainali za Afcon 2019.
Alisema anakumbuka wakati akicheza soka waliitwa Ikulu mwaka 1994, ambapo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi aliwaandalia tafrija fupi kuwapongeza kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Chalenji.
Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Oscar Milambo, alisema tayari TFF ina programu ya muda mfupi, mrefu na Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike ameshazipitia na wamejadili kwa ajili ya utekelezaji.
Milambo alisema ujenzi wa timu imara za Taifa unaanzia ngazi za chini na amewataka wadau wote kuhakikisha Taifa Stars mpya ya kufuzu fainali za Afrika 2021 na Dunia 2022 inapata maandalizi ya kutosha.
“Kama ujenzi wa nyumba unaanzia kwenye msingi, basi na sisi tumeshaanza kujenga msingi imara kwa hizi timu za vijana, tayari mashindano ya vijana yapo kinachohitajika ni kuviendeleza vipaji vinavyopatikana,” alisema Milambo ambaye ni kocha wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Nchini, Yusuph Singo alisema watapokea mpango kazi wa TFF wa mwaka mzima ambao unapaswa kupelekwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
"Siyo TFF pekee, vyama na mashirikisho yote vinapaswa kupeleka mipango kazi yao ya mwaka mzima BMT wao wanaiwasilisha kwetu," alisema Singo.
Alisema Serikali ina utaratibu wa kuunga mkono vyama vyote katika maeneo yote yanayohusika kuanzia ufundi, fedha, usalama.
"Hata kwa Stars, kuna vitu vingi tunafanya, ingawa suala la maandalizi ya awali yanafanywa na shirikisho kwa kushirikiana na wenzao wa kimataifa, kabla ya kuja kwetu.
"Hata kwenye maandalizi ya Afcon, Serikali tumehusika na baada ya hii ya sasa, tutashirikiana kwa ile ya mwaka 2021. Jambo la msingi ni mpango kazi tu," alisem Singo.
Taifa Stars inashika nafasi ya pili Kundi L ikiwa na pointi tano, baada ya kutoka sare ya 1-1 na Lesotho, ilitoka suluhu na Uganda ilifungwa 3-0 na Cape Verde ugenini kabla ya kuilaza 2-0 Dar es Salaam.