Chapecoense kucheza na Barcelona Agosti 7 mechi ya kumbukumbu ya vifo vya ajali ya ndege

Muktasari:
Mechi hiyo ni kumbukumbu ya vifo vya wachezaji 71 waliofariki dunia mwaka jana kutokana na ajali ya ndege.
Madrid, Hispania. Klabu ya Barcelona wataikaribisha timu ya Chapecoense katika mechi ya kuwania taji la Joan Gamper mechi itakayochezwa kwenye dimba la Camp Nou Agosti 7.
Mechi hiyo ni kumbukumbu ya vifo vya wachezaji 71 waliofariki dunia mwaka jana kutokana na ajali ya ndege.
Miamba hao wa La Liga wamewakaribisha Chapecoense ili kucheza mechi hiyo kabla ya msimu kuanza ili kukumbuka vifo cha wachezaji wenzao, waandishi wa habari pamoja na benchi la ufundi waliopoteza maisha kwenye ajaili hiyo.
Hata hivyo, watu watatu pekee waliokuwamo kwenye ndege hiyo walisalimika ambao ni Neto, Alan Ruschel na Jackson Follmann lakini walipata majeraha na wengine kuvunjika pamoja na kupata madhara kwenye moyo.
Barcelona na Chapecoense watacheza mechi huyo kuwaenzi wenzao ikiwa ni mashindano ya 52 kufanyika huku lengo ikiwa ni kuwapa moyo na kujiimarisha upya.