Chama, Bwalya wapindua meza kibabe

Muktasari:

  • Zambia inashika mkia wa kundi H la kuwania kufuzu fainali za Afcon ikiwa na pointi tatu huku Algeria ikiongoza na pointi zake 10, Zimbabwe iko nafasi ya pili na pointi tano ilizokusanya wakati nafasi ya tatu wako Botswana walio na pointi nne.

Baada ya kuenguliwa katika kikosi cha Zambia miezi minne iliyopita, viungo wa Simba, Rally Bwalya na Clatous Chama wamerudishwa kundini katika timu hiyo inayojiandaa na mechi mbili za kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani dhidi ya Algeria na Zimbabwe mwishoni mwa mwezi huu.

Bwalya na Chama hawakujumuishwa katika kikosi cha Zambia kilichocheza dhidi ya Botswana, Novemba mwaka jana ambapo walipoteza moja kwa bao 1-0 na kushinda nyingine kwa mabao 2-1, matokeo yaliyoiweka katika nafasi ngumu ya kufuzu fainali zijazo za Afcon.

Lakini baada ya kutoa mchango mkubwa katika kikosi cha Simba kwenye mechi mbili za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita na Al Ahly ambazo kila moja waliibuka na ushindi wa bao 1-0, Chama na Bwalya safari hii wamejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 33 wa timu ya taifa ya nchi hiyo 'Chipolopolo' kitakachocheza nyumbani dhidi ya Algeria, Machi 25 na kisha kuikabili ugenini Zimbabwe, Machi 29.

Nyota wawili wa Red Bull Salzburg ya Austria, Enock Mwepu na Patson Daka ni miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi hicho cha Zambia kilichosheheni idadi kubwa ya nyota wanaocheza soka katika klabu za ndani za nchi hiyo lakini pia kocha Micho amemjumuisha Fashion Sakala anayeitumikia KV Oostende ya Ubelgiji.

Kama ilivyotarajiwa, kocha Micho amewajumuisha nyota wawili wanaounda moyo wa ulinzi wa TP Mazembe, Tandi Mwape na Kabaso Chongo lakini pia hakusita kuliweka katika orodha jina la mshambuliaji aliyewahi kuhusishwa na Simba, Justin Shonga anayechezea Cape Town City ya Afrika Kusini.

Kikosi hicho cha wachezaji 33 kinaundwa na makipa Allan Chibwe wa Green Eagles, Cyril Chibwe (Polokwane City) na Lameck Siame (Kabwe Warriors).

Mabeki walioitwa ni Kabaso Chongo, Tandi Mwape (TP Mazembe), Luka Banda (Napsa Stars), Adrian Chama, Clement Mulashi (Zesco United), Golden Mafwenta (Buildcon), Dominic Chanda (Kabwe Warriors), Benedict Chepeshi (Red Arrows) na Zachariah Chilongoshi (Power Dynamos).

Nyota wa nafasi ya kiungo walioitwa ni Enock Mwepu (Red Bull Salzburg), Nathan Sinkala (Stellenbosch), Salulani Phiri (Polokwane City), Kings Kangwa (Arsenal Tula), Clatous Chama, Rally Bwalya (Simba), Paul Katema (Red Arrows), Benson Sakala na Spencer Sautu (Power Dynamos).

Kwa upande wa ushambuliaji, walioitwa ni Patson Daka (Redbull Salzburg), Fashion Sakala (Oostende), Gamphani Lungu (SuperSport United), Lubambo Musonda (Slask Wroclaw), Roderick Kabwe (Black Leopards), Augustine Mulenga (Amazulu), Justin Shonga (Cape town City), Brian Mwila (Buildcon), Moses Phiri (Zanaco), Collins Sikombe (Lusaka Dynamos), Amity Shamende (Green Eagles)

Wakati Chama na Bwalya wakijumuishwa katika kikosi cha Zambia, nyota mwingine wa Simba, Lwanga Taddeo naye ametajwa katika kikosi cha wachezaji 31 wa Uganda kinachojiandaa na mechi mbili za kuwania kufuzu Afcon dhidi ya Burkina Faso na Malawi.

Kikosi hicho cha Uganda pia kimewajumuisha nyota wengine wawili wanaocheza soka la kulipwa hapa Tanzania ambao ni kipa, Mathias Kigonya na beki wa kulia, Wadada Nico Wakiro ambao wanaitumikia Azam FC

Wachezaji wanaounda kikosi cha Uganda ni makipa Denis Onyango (Mamelodi Sundowns), Salim Jamal Magoola (Al Hilal), Mathias Kigonya (Azam) na Charles Lukwago (KCCA FC) wakati mabeki ni Nico Wakiro Wadada(Azam FC), Elvis Bwomono (South End), Bevis Mugabi (Motherwell), Murushid Juuko (Express FC), Musitafa Kiiza(DC Montreal), Joseph Ochaya (TP Mazembe), Timothy Dennis Awany (FC Ashdod), Ronald Mukiibi(Ostersunds), Halid Lwaliwa (Vipers SC) na Garvin Kizito (SC Villa).

Viungo walioitwa ni Khalid Aucho (Misr El Makkasa), Mike Azira (New Mexixo United), William Kizito Luwagga (Hapoel Kfar Saba), Allan Okello (AC Paradou),  Allan Kyambadde (El Gouna), Moses Waiswa (SuperSport United), Taddeo Lwanga (Simba SC), Abdu Lumala (Pyramids FC) na Bobosi Byaruhanga (Vipers SC)

Kwa washambuliaji, walioitwa ni Uche Ikpeazu Mubiru (Wycombe Wanderers), Fahad Bayo (FC Ashdod), Daniel Isiagi(Jomo Cosmos), Faruku Miya (Konyaspor) Yunus Ssentamu (Vipers), Emmanuel Okwi (Al Ittihad Alexandria), Patrick Kaddu (Youssoufia Berrechid)